Habari

Ethiopia wazindua treni ya kisasa mjini Addis Ababa

Huduma ya treni ya kisasa imezinduliwa rasmi September 21 jijini Addis Ababa, Ethiopia.

radar_addis_ababa_new_train

Mradi huo mkubwa uliogharimu dola za kimarekani milioni 470 ulifadhiliwa na China Exim. Siku ya Jumapili ilikuwa nzuri kwa wakazi wa Addis Ababa kwani walipata usafiri wa bure wakati wa uzinduzi wa treni hiyo ya kisasa.

Treni hiyo itakuwa ikibeba watu 15,000 kwa kila saa moja kuelekea upande mmoja wa jiji. Inamaanisha inaweza kuzunguka mara nne, kwani spidi yake ni kilomita 70 kwa saa.

treni

Mradi huu umewezekana kutokana na maandalizi ya kutosha hasa kwenye sekta ya umeme nchini humo ambako wameweza kujenga mfumo unaozalisha megawati 6000. 

Wameweza kujenga Grand Renaissance dam, mradi wa sabini kwa ukubwa wa kutengeneza umeme. Nchi hii inakuwa kiuchumi kutokana na wawekazaji wengi kuamua kuwekeza nchini humo.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents