Tupo Nawe

Ethiopia: Waziri Mkuu ashinda tuzo ya amani ya Nobel, awapiku zaidi ya washiriki 300 waliyochaguliwa

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameshinda tuzo ya amani ya ‘Nobel Peace Prize’ kwa mwaka 2019. Waziri mkuu huyo ametunukiwa tuzo kwa jitihada zake za kuleta amani na ushirikiano wa kimataifa.

Image result for Ethiopia Abiy Ahmed Nobel

Mkataba wa amani ulisainiwa mwaka jana, mgogoro wa kivita na nchi jirani uliochukua karibu miaka 20 tangu mwaka 1998-2000 . Ahmed alitajwa kuwa mshindi wa 100 wa Nobel Peace Prize huko Oslo.

Jumla ya washiriki 301 waliochaguliwa katika tuzo hizo zenye hadhi kubwa, washiriki 223 ni watu binafsi na kampuni 78 .

Tayari watu walikuwa wamekisia nani angeshinda tuzo. Chini ya kanuni za asasi ya Nobel , washiriki waliotajwa majina yao hayaruhusiwi kuchapishwa kwa miaka 50.

Hizi ni Tuzo gani?

Mwanasayansi wa Sweden, Alfred Nobel alianzisha kwa mapenzi yake tuzo hizi mwaka 1895 Hutolewa tuzo tano, kwenye Kemia, fasihi andishi, tuzo ya amani,Fizikia na Fiziolojia(Dawa).

Abiy Ahmed ni nani?

Baada ya Ahmed kuwa waziri mkuu mwezi Aprili, 2018, Bwana Abiy alianzisha mabadiliko katika taifa taifa la Ethiopia. Ahmed aliwaachia huru maelfu ya wanaharakati waliokuwa gerezani na wale walio katika uhamishoni kurejea nyumbani.

Jambo la muhimu zaidi waziri mkuu huyu alisaini mkataba na nchi jirani ya Eritrea kumaliza mgogoro baina yao ambao ulichukua miongo miwili.

Lakini mabadiliko au harakati alizozifanya zilipelekea nchi hiyo kutokuwa na utulivu na watu milioni 2.5 walilazimika kuhama makazi zao kutokana na vurugu.

Kwa nini Abiy Ahmed alishinda?

Kamati ya tuzo hiyo ya Norwal katika hutuba yao , walisema kuwa bwana Abiy ametunukiwa tuzo hiyo ya heshima kwa kufanikiwa kutatua mgogoro wa mipaka na nchi jirani ya Eritrea.

“Tuzo hiyo ina maana kuwa imetambua juhudi za washirika wanaotaka amani na makubaliano nchini Ethiopia , Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla,” waandaji walisema.

Waliowahi kupata tuzo za amani za Nobel

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2009, kwa jitihada za kuimarisha diplomasia ya kimataifa na ushirikiano baina ya watu.

Rais mwingine wa Marekani, Jimmy Carter (2002).

Washindi kutoka Afrika wa Tuzo za Nobelraia wa DRC Denis Mukwege ashinda Tuzo ya Amani ya Nobel

Raia wa DRC Denis Mukwege ndie mshinda wa tuzo ya Amani ya Nobel kwa mwaka 2018

Mwaka jana raia wa DRC Denis Mukwege ashinda Tuzo ya Amani ya Nobel kwa juhudi zake kukabiliana na udhalilishaji wa kingono nchini humo.

Denis Mukwege ni mtaalamu wa masuala ya uzazi ya wanawake ambaye amekuwa akifanya kazi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Yeye na wenzake wamewatibu na kuwafanyia upasuaji wa kurekebisha viungo maelfu ya waathiriwa wa udhalilishaji wa kingono, wengi ambao walidhalilishwa vitani.

Mukwege ametunukiwa tuzo hiyo pamoja na Nadia Murad.

Kamati ya Nobel imesema yeye “ni mmoja wa wasichana na wanawake takriban 3,000 wa jamii ya Yazidi ambao ni waathiriwa wa ubakaji na udhalilishaji wa kingono uliotekelezwa na wapiganaji wa Islamic State.”

Tutu, Desmond Mpilu (Afrika Kusini) -Alipata tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1984: Ni mmoja kati ya wanaharakati wa haki za binaadam , alipata tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kumaliliza vitendo vya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini .Alikuwa Kiongozi wa kwanza mweusi wa madhehebu ya Anglikana wa mji wa Cape town na Johannesburg. Aliitwa sauti ya wasio na sauti, alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa kibaguzi.Nelson Mandela alipokuwa Rais wa kwanza mweusi nchi humo, alimteua Tutu kuwa mwenyekiti wa tume ya ukweli na maridhiano.

Zewail, Ahmed Hassan (Misri)-Alipata tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka 1999 kuhusu mabadiliko ya kemikali.Zewail alikuwa mwanasayansi wa kwanza mwenye asili ya kiarabu kupata tuzo hiyo.

Johnson Sirleaf, Ellen (Liberia)-Alipata tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2011 kutokana na juhudi za kupambania usalama wa wanawake , haki za wanawake na ushiriki wa wanawake katika kazi ya kuijenga amani ya Liberia.Mwanamama huyu ni rais wa kwanza mwanamke barani Afrika aliyechaguliwa kidemokrasia,alichangia sana kuimarisha amani ya Liberia na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kuimarisha nafasi za wanawake.

Wangari Maathai (Kenya)-Alitunukiwa tuzo ya amani ya Nobel , Mama Wangari aliweka jitihada zake katika kupigania haki za binaadamu na haki za wanawake .Pia alipigania utunzaji wa mazingira , si Kenya pekee bali Afrika alianzisha kampeni ya kupanda miti na kuwahamasisha wengine kuwajibika kutunza mazingira yao, serikali yao inayowaongoza, maisha yao na mustakabali wa maisha yao.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW