Habari

Ethiopia yatoa bosi mpya wa WHO

Tedros Adhanom Ghebreyesus kutoka nchini Ethiopia anatarajiwa kuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani (WHO).

Endapo Tedros (52) atafanikiwa kukalia kiti hicho kuanzia Julai 1, mwaka huu baada ya mkurugenzi wa sasa Margaret Chan kumaliza muda wake wa miaka 10 ya utumishi ifikapo mwezi Juni mwishoni, atakuwa ni mtu wa kwanza kutoka Afrika kushika nafasi hiyo.

Adhanom amepata nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura 186 na wanachama wa shirika hilo wakimtaka awe mkuugenzi mpya.

Kiongozi huyo amewahi kuwa waziri wa afya wa Ethiopia kuanzia mwaka 2005 mpaka 2012, lakini pia amewahi kuwa waziri wa mambo ya nje kuanzia 2012 hadi 2016.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents