Michezo

Etoile Sahel yaiadhibu Zesco ya Lwandamina klabu bingwa Afrika

Klabu ya Etoile Sahel ya nchini Tunisia ikiwa nyumbani imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 1 dhidi ya timu ya Zesco United ya Zambia mchezo wa kundi D wa michuano ya klabu bingwa barani Afrika uliyopigwa hapo jana siku ya Jumatano.

Zesco United inayonolewa na aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga, George Lwandamina imekubali kipigo hicho wakiwa ugenini wakati mabao ya kifungwa na Alaya Brigui dakika ya 46, Amr Marei dakika ya 56 na lakufutia machozi kwa upande wa Wazambia hao likipachikwa na Lazarous Kambole dakika 91 za mchezo.

Kwa matokeo hayo yanawafanya mabingwa hao wazamani wa Afrika, Etoile kujiunga na Mbabane Swallows ya Swaziland kwenye msukani wa kuongoza kundi hilo la D ikiwa timu zote zimejikusanyia alama nne.

Wakati klabu ya Zesco United ikiangukia nafasi ya tatu huku Primeiro Agosto ya Angola ikiburuza mkia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents