MichezoUncategorized

Europa League: Arsenal hakuna kuremba, Dortmund yabebwa na wachezaji wa Chelsea

Usiku wa kuamkia leo michezo 16 ya kombe la Uefa Europa League imechezwa katika hatua ya timu 32 bora. Miongoni mwa mechi zilizochezwa ni Ostersunds ya Sweden dhidi ya Arsenal ambao wlikuwa wageni wa mchezo huo.

Katika mchezo huo Arsenal walipata ushindi wa mabao 3-0. Mabao hayo yalifungwa na Nacho Monreal dakika ya 13, Mesut Ozil 58 na bao la kujifunga la Sotirios Papagiannopoulos kwenye dakika ya 24.

Katika mchezo mwingine uliochezwa Borussia Dortmund ambao walikuwa nyumbani walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3 dhidi ya mawili ya Atalanta. Mabao ya Dortmund yalifungwa na wachezaji wa zamani wa Chelsea, André Schürrle dakika ya 30 na Michy Batshuayi sliyefunga mara mbili, katika dakika ya 65 na 90.

Nao Atalanta walipata mabao yao yote mawili kupitia kwa Josip Iličić, akika ya 51 na 56. Haya hapa chini ni matokeo ya mechi nyingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents