Michezo

Europa League: Griezmann awabana Arsenal nyumbani, Marseille wapeta

Usiku wa jana michezo ya nusu fainali ya kombe la Europa League imechezwa ambapo Arsenal wakiwa kwenye uwanja wa Emirates wametoka sare ya kufungana bao 1-1 na Atletico Madrid ya Hispania.

Arsenal ndio walikuwa wakwanza kufunga goli lao kupitia kwa acazette dakika ya 61 wakati bao la Atletico lilifungwa na Antoine Griezmann dakika ya 82.

Katika mchezo huo Atletico walilazimika kucheza wachezaji 10 uwanjani baada ya beki wao Sime Vrsaljko kuonyeshwa kadi nyekundu katiaka dakika ya 10 ya kipindi cha kwanza.

Wakati huo huo kwenye nusu fainali nyingine, Olympique de Marseille ya Ufaransa walikuwa nyumbani walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya RB Salzburg ya Austria.


Mabao ya Marseille yalifungwa na Thauvin (15) na Clinton N’jie (63).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents