MichezoUncategorized

Everton vs Gor Mahia: SportPesa kutoa tiketi 4000 bure kwa Watanzania (+Video)

Kuelekea mchezo wa Everton dhidi ya Gor Mahia Kampuni ya kubashiri ya SportPesa imetangaza kutoa tiketi 4000 bure kwa Watanzania ili waweze kuingia Uwanja wa taifa kushuhudia mtanange huo ambao utafanyika mwezi ujao julai 13 kunako dimba la taifa jijini Dar es salaam.

Viongozi wa SportPesa katikati,Bodi ya Utalii kulia na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kushoto.

Akithibitisha taarifa hizo Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania Bwana Abbas Tarimba amesema utoaji wa Tiketi hizo utakuwa kwa Watanzania wote wapenda soka kwani ni kama zawadi ingawaje kutakuwa na vigezo na masharti kwa utoaji wa tiketi.

Kuelekea mechi hii ya Everton dhidi ya Gor Mahia kampuni yetu itatoa tiketi 4000 ili Watanzania waweze kushudia mtanange huo pale Taifa,” amesema Abbas Tarimba.

Akizungumza na waandishi wa habari Bw. Tarimba amesema vigezo vya kujishindia tiketi hizo vitakuwa ni rahisi kwani itatakiwa mtu kutuma Screenshots za codes alizotumiwa na SportPesa baada ya Kubeti na kisha posti screenshot hizo kwenye ukurasa wako wa mitandao ya kijamii (Facebook/Twitter/Instagram) na kisha watag SportPesa na ambatanisha na Hashtag ya #EvertoninTz kwa kufanya hivyo utakuwa umejipatia tiketi yako ya VIP kuwashuhudia Everton, Tahadhari kumbuka kigezo cha kwanza ni lazima uwafollow Sportpesa kwenye mitandao yao ya kijamii kama upo Facebook like ukurasa wao hapa HAPA  na kama upo Twitter wafollow HAPA na kama upo Instagram wafollow HAPA ujiwekee nafasi ya kujishindia tiketi.

Kwa upande mwingine Bwana Tarimba amesema kwa wale watakao nunua tiketi zitauzwa kwa bei isiyozidi Tsh 10,000 hii yote ni kufanya watu waburudike vya kutosha siku hiyo.

Hata hivyo kwa upande wa Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) wameyabariki mashindano hayo kwa kusema kuwa yataongeza hamasa kwa wachezaji wa ndani ya nchi na kuwataka Watanzania kiujumla kujitokeza kwa wingi kushuhudia mtanange huo.

Tunaamini ushirikiano wa SportPesa na ujio wa Everton utasaidia ukuaji wa soka nchini hivyo nawaomba Watanzania tuwapokee Everton kwa mikono miwili tuje kwa wingi tuione burudani kutoka EPL kila mtu atavaa jezi anayoipenda itakuwa burudani tuu,” amesema Salum Madadi Mkurugenzi wa Ufundi TFF.

Sportpesa ambao ndiyo wadhamini wa Klabu ya Everton na Gor Mahia wamezikutanisha klabu hizo baada ya mchujo wao mrefu kupitia mshindi wa kombe la Sportpesa Super Cup ambapo tuliona timu nne kutoka Tanzania zikitupwa nje ya michuano hiyo mwanzoni mwa mwezi uliopita.

 

By Godfrey Mgallah

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents