Michezo

Everton yaendelea kuonyesha jeuri ya fedha kwenye usajili

Klabu ya soka ya Everton ya Uingereza imeendelea kutikisa katika soko la usajili msimu huu.

Timu hiyo ambayo wiki iliyopita ilijitupa katika uwanja wa taifa jijini Dar ese Salaam kucheza na Gor Mahia ya Kenya, imefanikiwa kumsajili winga machachari wa Southampton, Cuco Martina.

Everton imemsajili mchezaji huyo kwa mkataba wa miaka mitatu. Baada ya kufanyika usajili huo kocha wa Everton, Ronald Koeman ameonekana kufurahishwa na usajii huo kwa kusema, “Ni mchezaji ambaye ataimarisha kikosi chetu na kuwa na uwezo wa kucheza katika nafasi tofauti wakati inahitajika pia.”

Cuco ni mchezaji wa sita kusajiliwa na Everton msimu huu baada ya Jordan Pickford, Davy Klaassen, Michael Keane, Wayne Rooney na Sandro Ramirez. Mchezaji huyo raia wa Uholanzi alijiunga na Southampton mwaka 2015 akitokea FC Twente.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents