Michezo

Everton yajaribu zali la kumn’goa beki wa Barcelona

Everton imewasilisha ombi la paundi milioni 40 kumsaini kiungo wa kati wa Napoli, Allan, 29, lakini klabu hiyo inataka dau la paundi milioni 60 kumuuza raia huyo wa Brazil. (Il Mattino – in Italian)

Everton open talks with Barcelona over £17.4m deal for Jean-Clair ...

The Toffees pia wamewasilisha ombi la paundi milioni 22 kwa Barcelona kumnunua beki wao, raia wa Ufaransa Jean-Claire Todibo ,20, ambaye kwa sasa anatumikia Schalke 04 kwa mkopo. Yaipa Barcelona siku chache za kutoa majibu ya ombi lao (Mail)Manchester United kumuongezea kandarasi kipa wa England Dean Henderson

Manchester United kumuongezea kandarasi kipa wa England Dean Henderson

Manchester United itamuongezea kandarasi kipa wa England Dean Henderson, 23 ili kumruhusi kumaliza msimu wake na klabu ya Sheffield United huku kandarasi yake ikitarajiwa kukamilika mwezi Juni. (Telegraph)

Mmiliki wa Bournemouth Maxim Demin karibu aiuze klabu hiyo kwa mfanyabiashara wa Saudia mnamo mwezi Januari, kabla ya makubaliano hayo kugonga mwamba kuhusiana na thamani ya klabu hiyo. (90min)Phillipe Coutinho

Kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Bayern Munich huenda asicheze tena baada ya klabu hiyo ya Bundesliga kuamua kutomsaini kwa mktaba wa kudumu kutoka Barcelona, na sasa ananyatiwa na Chelsea, Arsenal na Tottenham. (Sky Sports)

Chelsea imeamua kutotumia kifungu chake cha sheria dhidi ya winga wa Ivory Coast Jeremie Boga ,20, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kwenda kuichezea klabu ya Napoli. (Guardian)Mauro Icardi

Mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icardi anakaribia kuhamia PSG

Mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Mauro Icardi, 27, anakaribia kuhamia katika klabu ya Paris St-Germain kwa dau la £54m. (ESPN)

Paris St-Germain inafanya mazungumzo na Arsenal katika jaribio la kumsaini mashambuliaji wa klabu hiyo Pierre-Emerick Aubameyang, 30, kwa£34m. (Todofichajes)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents