Michezo

Everton yashinda 2-0 Europa League

Klabu ya Everton ya Uingereza inayodhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sportpesa imefanikiwa kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya Europa League baada ya kuchomoza na ushindi wa jumla ya mabao 2-0 dhidi ya Hajduk Split .


Magoli ya, Michael Keane na Idrissa Gueye yalitosha kabisa kuwafanya vijana wa Toffees kutoka kifuambele mbele ya mashabiki wa Hajduk waliyokuwa wamejaa uwanjani wakiipasapoti timu yao huku wakileta vurugu hadi kupelekea mpira kusimama kwa muda katika dakika 45 za kwanza za mchezo huo.

Mlindalango wa Everton, Jordan Pickford aliyesajiliwa kwa dau la pauni milioni 30 aliisaidia timu yake kwa kuokoa michomo kadhaa iliyokuwa ikilenga golini hasa kutoka kwa mchezaji, Franck Ohandza.

Meneje wa Everton mholanzi, Ronald Koeman sasa anakiandaa kikosi chake kwaajili ya mchezo wa marudiano huko Croatia Alhamisi ya wiki ijayo na matokeo ya ushindi, suluhu ama bao moja yatatosha kusonga mbele katika michuano hiyo ya Europa.

“Nilikuwa na furaha sana katika kipindi chakwanza na furaha ilipotea kipindi chapili kwa kuwa tulipata nafasi nyingi ya kufunga magoli lakini tulishindwa kuzitumia nafasi hizo”, alisema mholanzi huyo.

Katika michezo mingine iliyochezwa ya michuano hiyo klabu ya Ajax imefanikiwa kuchomoza na ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Norwegian.

Kikosi cha Ajax kikiwa kinashangilia

Ajax ambayo msimu uliyomalizika ilifungwa na Manchester United katika hatua ya fainali ya michuano hiyo imeonekana kufanya vizuri mbele ya kocha wao mgeni Marcel Keizer.

Matokeo ya baadhi ya michezo mingine

 

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents