Everton yavutwa shati mbele ya Walcott Goodison Park

Timu ya Everton hii leo imeshuka katika uwanja wake wa nyumba wa Goodson Park huku ikiwa na mchezaji wake mpya iliyomsajili kutoka Arsenal, Walcott na kukubali kutoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya West Brom.

Katika mchezo huo uliyokuwa na mvuto na kushambuliana kila pande timu ya West Brom ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa mchezaji wake Rodriguez kunako dakika ya 7 kabla ya Oumar Niasse kuisawazishia the Toffees katika dakika ya 70.

Kwa matokeo hayo sasa Everton inakuwa katika nafasi ya tisa mwa msimamo wa ligi ya England kwa kuwa na jumla ya pointi 28 wakati West Brom wakiwa katika nafasi ya 19 kwa kuwa na alama 20.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW