Ex wa Kylie Jenner, Tyga anataka kufanya DNA na Stormi Webster

Wiki ilililopita, Kylie Jenner na mpenzi wake Travis Scott walimkaribisha binti yao mzuri, Stormi Webster na kutangaza kuzaliwa kwa mtoto huyo kwa ulimwengu kupitia mtandao wa Instagram.

Kwa mujibu wa Radar online, Tyga anadai kutaka kufanya DNA kwa sababu anaamini Stormi anaweza kuwa mtoto wake na sio Travis.

“Tyga inataka kufanya DNA kwa sababu anafikiria kuwa kuna uwezekano kuwa mtoto huyo anaweza kuwa ni wa kwake,” Source imeongezea.

Kylie na Tyga walikuwa bado ni wapenzi miezi tisa kabla ya Stormi kuzaliwa japo kuwa wawili hao walitangaaza kuachana mwezi Aprili 2017.

“Tyga aliwaambia marafiki zake kuwa bado ana mahausiano na Kylie miezi tisa iliyopita na ndiyo wakati kylie alipata mimba ya mtoto huyo,” chanzo kiliongezea.

Siku ya Jumatatu Radar online waliiambia Hollywood Life kwamba Tyga anataka kukutana na mtoto huyo (Stormi).

Source huyo ilisema kwamba “Tyga ana maswali mengi na muhimu zaidi bado anajiuliza kama kuna uwezekan kama mtoto huyo anaweza kuwa wake.” Tyga anamkumbuka Kylie sasa zaidi kuliko hapo awali, anataka kweli kukutana na mtoto na anataka ufafanuzi fulani.”

Ikiwa Stormi ni mwanae basi msanii huyo anapaswa kuwa na uhakika ili aweze kuamka na kuwa baba bora.”

Mtandao wa Vogue unao jiusisha na mambo ya fasheni linasema kuwa mnamo Septemba mwaka jana, Tyga alikuwa akifanya ununuzi huko jijini Los Angeles na alisikika akiwaambia mashabiki, “Hell nah that’s my kid” alipoulizwa kuhusu mimba ya Ex wake Kylie Jenner.

Tyga hapo awali aliposti video flani hivi na kisha kufuta katika mtandao wa Snapchat ambapo katika video hiyo alikuwa akidai kuwa mtoto wa Kylie ni mtoto wake.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW