Exclusive 255: John Mahundi alizungumzia No Name, kumtoa tena Crazy GK, kuhusu kupata identity ya muziki wa Tanzania

John Mahundi ni producer na member wa kundi la No Name linalojumisha maproducer akiwemo P-Funk Majani, Dunga, Lamar na Karabani. Pia ni msemaji wa kundi hilo na kwenye EXCLUSIVE 255, amezungumza na Bongo5 kuhusu masuala mbalimbali.

Kuhusu kinachofuata kwa No Name

Sasa hivi tupo kwenye harakati ya kurelease single ya pili, itatoka very soon nadhani ndani ya wiki, wiki mbili itakuwa imeshatoka. Tumeshamaliza kuirecord na tunaifanyia video pia.

Kuhusu video ya single yao ya kwanza

Kulikuwa na vitu ambavyo Adam alikuwa anamalizia, kwahiyo inabidi tukutane na Adam kuangalia kitu gani kinahitajika.

No Name
No Name

Kuhusu mpango wa albam yao

Albam nayo ilikuwa tufanye ipo lakini tunasogeza mbele kidogo, tutakuwa tukirelease single nyingi kidogo hapa katikati ili kupush project yenyewe na kupush jina la group na kuangalia market ina respond vipi ndio tutakwenda kwenye upande wa albam.

Kuhusu tour ya No Name

Yes, we are thinking about it lakini bado hatujafanya confirmation lakini definitely zote hizo zipo kwenye plan na tour tunafikiria sio Dar tu, sio Tanzania tu, tunataka kutoka nje ya nchi pia.

Kuhusu nani ni executive producer katika kutengeneza nyimbo zao

Wote ni executives, wote tunaiown project kikamilifu, so I guess ni wote.

Kuhusu kama atamrudisha tena King Grazy GK

Actually tuna nyimbo tatu tayari na GK na very soon na zenyewe zitatoka. Kuna possibility kubwa sana ya kurudi kufanya ngoma AY, FA , GK, actually tulifanya moja hatujaifinalize tu. Kuna nyimbo amefanya na Pauline Zongo halafu kuna nyingine amefanya mwenyewe.

Kuhusu Tanzania kuwa na muziki wenye identity yake

Cha kwanza inabidi tuangalie ndani yaani utamaduni wetu, nyimbo zetu za zamani na kujaribu kutafuta identity kwasababu kuna tendency ya wanamuziki na hata maproducer kutengeneza kile wanasikia kutoka west kwa mfano Nigeria muziki sasa hivi ni mkubwa unakuta watu wengine wanajaribu kutengeneza production za kinaijeria, kuna mambo ya euro dance, trans music za Europe. Tunajaribu kufuata direction za watu wengine hatujitahidi sana kuangalia kitu gani sisi wenyewe tunacho ndani ambacho tunaweza tukakitumia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents