Burudani

Exclusive: AT aizungumzia show yake ijayo ya nchini Uingereza

November 3 mwaka huu mfalme mpya wa mduara nchini Tanzania AT atafanya show nchini Uingereza. Tumefanya naye mahojiano kuhusiana na jinsi alivyojiandaa na nini anategemea kufanya.

“Kikubwa zaidi kwamba najua watu walikuwa wanafahamu muda mrefu ujio wangu kule niweze kufika lakini hivi sasa imefika nachosema kwamba niwaahidi watu wengi wameenda kufanya show lakini mimi nataka ya tofauti ili leo na kesho waweze kutamani show yangu na niweze kurejea tena kwahiyo kitu ninachowaahidi nitakwenda inshallah na ninaenda kufanya vizuri ambavyo wao hawajategemea,”alisema AT.

“Nitakachokifanya najua wengine wana wasi wasi kwamba wanasikia tu AT akiwa pande hizi anafanya hivi na hivi wanahitaji kuona, kwahiyo mimi naamini kwamba Mungu akijalia niwe na uzima nitafanya kitu kizuri tena nawaaidi wata furahia.”

Aliendelea, “Safari yangu ni ya mwezi mmoja na nitafanya show UK na kawaida ukifanya show vizuri basi nyingine zitajitokeza unaweza ukafanya Scotland, yaani vyote vinaweza vikatokea lakini kikubwa ni nachoenda kufanya pale London.

Hii show naenda mwenyewe kutokana nikasema kwamba kuna vitu nataka kufanya kule kwasababu nataka kufanya show ambayo kama vile itahusisha watu ambao wapo ina maana hanihusu AT peke yangu halafu mtu anaelipa, anakuja nae anaona, maana yake hii show sio mpira unaingia ndani unalipa lakini huchezi, wewe unaangalia, lakini show unaingia unalipa na unacheza wewe nataka watu waenjoy.”

“Najua unaposafiri unajifunza,nakusoma, nataka nikasome watu wanaishi vipi ndugu zetu kule kuna nini na nini,inabidi nisome vitu vingine tofauti na music yaani ukiachia mbali na maisha totauti na music ili siku ya pili nikirudi hivi nijue nimeshapata elimu.”

Katika hatua nyingine AT aliongelea kuhusu kumalizia ngoma zake mbili alizozifanyia Tanga ambazo ni Muhogo na Nitafute.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents