Burudani ya Michezo Live

Exclusive Audio: Mabomu yatawala Mtwara, wananchi waingia tena mtaani kupinga ujenzi wa bomba la gesi

Habari kutoka mjini Mtwara zinadai kuwa hali si shwari baada polisi kulazimika kuingia mtaani kuwatawanya wananchi kwa mabomu wanaoandamana kufuatia kauli ya waziri wa nishati na madini, Sospeter Muhongo kwenye hotuba ya katiba ya wizara hiyo kuwa serikali itaendelea na zoezi la ujenzi wa bomu la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.

IMG_20130522_102325

Kazi zilizopangwa kutekelezwa kwenye mradi huo ni pamoja na: ujenzi wa mitambo miwili ya kusafisha gesi asilia katika maeneo ya Songo Songo (Lindi) na Mnazi Bay (Mtwara); ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Lindi na Mtwara hadi Dar es Salaam.

IMG_20130522_102338

Shilingi bilioni 63, sawa na dola za Marekani milioni 39.4 zitatumika.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mwananchi tuliyeongea naye kwa simu, hali bado si shwari mjini humo na maduka mengi yamefungwa pamoja na kusimama kwa shughuli nyingi.

Msikilize zaidi hapa.

Picha na jonaschaona.blogspot.com

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW