Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Exclusive Audio: MwanaFA na Ditto (Mashabiki wa Man U) wazungumzia kustaafu kwa Ferguson na hatma ya timu yao

Mwana FA na Lameck Ditto ni mashabiki damu damu wa mashetani wekundu, Manchester United walioshtushwa na uamuzi wa kocha mkongwe wa timu hiyo, Alex Ferguson kustaafu.

page

Ferguson aliyekuwa meneja wa timu hiyo tangu mwaka 1986 alitangaza jana kuwa anastaafu kuinoa timu hiyo.

Msanii wa THT, Lameck Ditto amesema habari za Fergie zilimshtua kwakuwa meneja huyo ana mchango mkubwa katika mafanikio ya timu hiyo. Akimzungumzia kocha wa Everton David Moyes ambaye anatarajiwa kutangazwa kama meneja mpya wa timu hiyo, Ditto amesema anapaswa kupewa muda kwakuwa Man U ni timu kubwa.

“Ukipewa ile timu kwa msimu mmoja tu, inaweza ikawa tabu kwa kocha kama Moyes ambaye ametoka katika timu ya Everton, bado ni timu ndogo kwa daraja kama la Manchester,” amesema Ditto.

Naye Mwana FA amesema kwa umri wa Fergie suala la kustaafu lilikuwa haliepukiki.

“Apparently Ilibidi ufike muda astaafu tu,” anasema Mwana FA. “Unajua kuna wakati mwingine alikuwa anafanya maamuzi unahisi babu kachoka, babu anahitaji kupumzika sasa. Fergie ni legend lakini tulikuwa tunajua utafika muda itabidi aachie nafasi watu wengine wafanye kazi.”

Mwana FA amesema Manchester United haiwezi kuwa kama ilivyo bila Fergie.

Wasikilize zaidi hapa.

Naye staa wa Uganda, Jose Chameleone ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook:

Just heard that Sir Alex Ferguson of Manchester United has retired . I don’t know alot about football but i know one thing, Fergie.. is more than a A LEGEND,he has 3 virtues that we ought to learn from ;Hardwork, loyalty and commitment,those 3 can take anyone places A true legend indeed…LEONE ISLAND FOREVER

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW