Burudani

Exclusive: Chidi Benz apanga kuandaa ‘Get Together’ ya wasanii wote Tanzania (Audio)

Chidi Benz amepanga kufanya tukio kubwa kwenye muziki ambalo halijawahi kufanyika Tanzania. Rapper huyo anataka kuwakutanisha wasanii wote wa Tanzania ambapo wataongea na kubalishana mawazo kuhusu muziki wa Tanzania, kula, kunywa na kuburudika pamoja.

Chidi Benz

“Nahitaji watu wote tukusanyike, tukutane kwa siku moja iwe kama get together party,” Chidi ameiambia Bongo5.

“Iwe kama concert lakini ya wasanii tupu, wasanii wote then tuongee kuhusu mipango, tuongee kuhusu muziki wetu unaenda wapi, umetoka wapi, wapi upo, kitu cha kufanyika kwa baadaye, kitu cha kufanyika kwa sasa hivi, kitu cha kufanyika kuokoa, kutanua zaidi, kufungua zaidi, kuupatia nafasi zaidi. Kwa wale ambao wako juu, kwa wale ambao wako chini, kwa wale ambao wametoa single, kwa wale ambao hawajatoa single. Ni miksa, kwa wasanii wote ambao wanataka kufanya muziki wetu wa Bongo Flava pamoja na Hip Hop na kila tu,” amesema Chidi.

Ameongeza kuwa party hiyo itawahusisha pia hata wasanii wa Tanzania wa nchi za nje ambapo amepanga kuwaunganisha kwa njia ya Skype na kwamba hadi sasa wasanii wote aliowapigia na kuwapa wazo hilo wamekubali kushiriki.

“Radio zote zitakuwepo, blog zote zitakuwepo, vyombo vya habari vyote vitakuwepo,” ameeleza Chidi na kuongea kuwa wasanii wote wa kike watahusika kwenye masuala ya kupika kama wafanyavyo kwenye familia na pia wanaume wakifanya shughuli za kiume.

“Wa kiume watakuwa busy kubeba makreti, soda nini, kuvunja kuni yaani tunataka kufanya vitu kitamaduni kama vile tunavyofanya nyumbani, kama vile tunavyofanya kwenye maharusi. Idea yangu nataka nione wasichana wote, nione Lady Jaydee, Ray C, Stara, Linah nani wamevaa khanga na vitenge wanakatakata vitu, wanapika, wanakaanga misosi. Na Diamond, Ommy Dimpoz, Richie Mavoko, Juma Nature, Mchizi Mox, MB Dogg nani kwa pamoja wanaenda kubeba makreti nini kuweka ndani, kusafisha, kupiga deki ukumbi kama nini, yaani kinyumbani.”

Amesema pia kutakuwepo na burudani mbalimbali ambapo wasanii watajitolea kuwaburudisha wenzao na kuongeza kuwa ameshaongea na wasanii wengi huku wengine akiendelea kuwapa taarifa. “Naendelea kuongea na wengine, naendelea kuwapigia simu wengine kuwafahamisha. Mpaka wote watakaposema sawa tuandae, tujue wapi tutafanyia, ukumbi gani tutafanyia na siku gani na kazi iende.”

Chidi amesema kuna imani mitaani kuwa yeye ni mtu mgomvi lakini huo si ukweli na kila msanii anafahamu kuwa yeye ni mtu wa watu na ndio maana ameamua kufanya mradi huo.

“Nachohitaji kiwekwe wazi ni kwamba sio kila point lazima watu waweke negative. Sio kila mtu akiongea kitu, watu waweke negative ‘Chidi anatafuta kiki tu, labda kaona yupo kimya’ hapana, vitu vingine ni positive. So nahitaji ushirikiano wa vyombo vya habari kuwasambazia watu na kuwafikishia watu habari na tuombe Mungu hiyo siku itokee na ifanyike.”

Msikilize zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents