Habari

Exclusive: Dayna amshitaki producer Sheddy Clever COSOTA kwa ‘kumuibia’ beat

Wengi tulidhani hili swala limeisha hasa baada ya wahusika wote kuzungumza akiwemo mlalamikaji Dayna Nyange, producer Sheddy Clever wa Burn Records aliyeitengeneza beat hiyo iliyoleta mzozo, na Diamond Platnumz aliyeitumia beat hiyo katika single yake mpya ambayo ni talk of the town ‘My Number One’.

sheddy2
Sheddy Clever na Diamond Platnumz

Sheddy Clever ameongea exclusive na Bongo5 na kusema kuwa pamoja na kuwa yeye ndiye producer na mmiliki wa beat hiyo iliyozua utata lakini Dayna amemshitaki COSOTA kwa kumuibia beat aliyotumia Diamond katika ‘My Number One’.

Sheddy amesema alipokea simu kutoka COSOTA na kupewa taarifa kuwa anahitajika kufika katika ofisi zao Jumatano hii (September 25) kwaajili ya kesi hiyo.

Haya ndio maelezo ya Sheddy Clever:

“Juzi ilikuwa tarehe 14 nimepigiwa simu na namba ngeni ambayo siijui wakajitambulisha wao ni COSOTA, nikaambiwa nabarua yangu pale njiifuate inipe muongozo kwamba nahitajika pale. Basi sikuwa nashaka wala na hofu yoyote kwasababu mi ni mtu ambaye nafanya kazi na COSOTA ni watu ambao wapo kwaajili ya kazi yangu ya muziki.

Kwahiyo nikaenda nimefata hiyo barua kuja kufungua ile barua ni kuhusu mambo ya Dayna. Dayna ameenda ameshtaki amesema kwamba ile beat ameibiwa kwahiyo mpaka dakika hii mi sielewi kwamba ana matatizo gani huyo dada anasema kwamba ile beat kaibiwa na je, unajua kwamba ni makosa kumuita mtu mwizi kwahiyo anaweza kufunguliwa mashtaka kwanini amuite mtu mwizi, je anauhakika gani au ushahidi gani ile beat kaibiwa.

Kwahiyo nimeambiwa niende tarehe 25 ili niende nikaskilize inakuwaje, kwahiyo mi ntaenda kuskiliza tarehe 25 tujue inakuwaje ili tuweze kupata muafaka wa hili swala sababu mi sipendi haya matatizo….kwasababu naona yeye anataka liwe tatizo kwasababu mi naona limeisha…mi nahisi linaendelea kuwa kubwa zaidi, kwahiyo kama yeye anahitaji liwe kubwa basi litakuwa kubwa zaidi kama anahitaji yaishe basi yaishe”.

Sheddy aliongeza kuwa toka Dayna aanze kulalamika kupitia mitandao hajawai kumtafuta hata mara moja ili angalau amuulize chochote, zaidi ya kusoma habari zote katika vyombo vya habari na mpaka alipokuja kupokea barua ya kuitwa COSOTA.

Sheddy amesema katika barua hiyo wameitwa yeye, Diamond Platnumz pamoja na meneja wa studio ya Burn Records aitwaye D.Manyuti. Hata hivyo Sheddy aliongeza kuwa Diamond amesema hatahudhuria.

Mpaka habari hii inaenda hewani nimejaribu kumtafuta Dayna Nyange ili kuthibitisha kama ni kweli alifikisha malalamiko yake COSOTA kuhusu swala hilo lakini simu yake haikupokelewa.

Msikilize Sheddy Clever

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents