Tia Kitu. Pata Vituuz!

Exclusive Details: Wema Sepetu ni tajiri kiasi gani?

Well, well, well! Hiki ni kitu ambacho kila mmoja anapenda kukifahamu. Wema Sepetu ni tajiri kiasi gani? Ni ngumu kusema exactly mrembo huyu ana shilingi ngapi benki, lakini mambo anayofanya yanatupa jibu la wazi kuwa, Wema ana mkwanja mrefu. Tangu mwezi Juni mwaka 2012 tumekua tukiona sura mpya ya kifedha zaidi ya star huyu. So hebu tuangalie mangapi makubwa yaliyohusisha fedha nyingi aliyoyafanya.

IMG_4951

1. Thamani ya nyumba yake

Wema Sepetu aliwaacha hoi watu wengi baada ya kuonesha nyumba yake mpya exclusively kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV. Alisema thamani ya nyumba yake hiyo ilifikia shilingi milioni 400 na hiyo ni tofauti na karibu shilingi milioni 30 za kuipamba ndani. Hiyo ilikuwa ni tarahe za mwanzo za mwezi June, 2012. Watu wengi walishtushwa na uwezo wa Wema muda huu na hata wengine kupelekea kuripoti wamba nyumba hiyo haikua yake na mengine mengi.

Sebule
Sebule
Sehemu ya nyumba hiyi
Sehemu ya nyumba hiyi
Wema Sepetu akielezea jambo
Wema Sepetu akielezea jambo
Wema na Zamaradi Mketema wa Clouds TV
Wema na Zamaradi Mketema wa Clouds TV

912

Sehemu ya nje ya nyumba
Sehemu ya nje ya nyumba

616

Dj Choka alikuwa miongoni mwa watu waliotembelea nyumba hiyo
Dj Choka alikuwa miongoni mwa watu waliotembelea nyumba hiyo

2. Uzinduzi wa filamu yake Superstar

Katika historia ya Bongo Movies, hakuna filamu iliyowahi kuwa na uzinduzi kama filamu ya Wema, Supastar, ambayo hata hivyo haijawahi kutoka mpaka leo. Katika uzinduzi huo, Wema alimdondosha muigizaji namba moja wa kike nchini Nigeria, Omotola Jalade ambaye alimpeleka kwenye event iliyofanyika Hyatt Regency, kati ya hoteli kubwa, maarufu na ghali jijini Dar es Salaam, na baadaye Giraffe Hotel Ocean View ambako watu mbalimbali walikutana kubadilishana mawazo na Omotola. Inasemekana Omotola hufanya appearance kwenye shughuli za watu kwa gharama kubwa sana na hivyo kwa Wema kuwa na uwezo wa kumleta mpaka hapa Tanzania, ni kumaanisha alitumia hela nyingi kwa event hiyo pamoja na kumgharamia safari ya omotola Jalade. Inasemekana alitumia zaidi ya milioni 30 kwa shughuli yake.

IMG_6117

Awali ulifanyika uzinduzi wa filamu hiyo yenye mastaa kibao akiwemo yeye mwenyewe, TID, Shetta, Mwinyi Machozi, Chaz Baba, Barnaba na wengine kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro ambako mastaa wote wa orodha A nchini walihudhuria huku Shaa na Shilole wakiwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza.

DSC_0075

Ben Kinyaiya na Irene Uwoya
Ben Kinyaiya na Irene Uwoya
Ray, Dr Cheni, Steve Nyerere nao walihudhuria
Ray, Dr Cheni, Steve Nyerere nao walihudhuria

DSC_0172

Shaa akitumbuiza kwenye uzinduzi huo
Shaa akitumbuiza kwenye uzinduzi huo
Shughuli nzima hiyo iliyofanyika mwishoni mwa mwezi June mwaka jana, ilitumia takriban shilingi milioni 40 zikiwemo gharama za kumlipa Omotola.

3. Gari anayomiliki

Kwa sasa Wema anamiliki gari aina ya AUDI Q7 ambayo thamani yake inafikia shilingi milioni 80 pamoja na Toyota Mark X ambayo thamani yake ni takriban shilingi milioni 30 na pia aliwahi kumiliki Lexus ambayo pia linagharimu takriban milioni 35 za kitanzania.

Wema akiwa na mkoko wake
Wema akiwa na mkoko wake

4. Thamani ya ofisi na kampuni yake, Endless Fame Films

February 21, Wema alifanya uzinduzi maalum wa ofisi za kampuni yake ya Endless Fame Films zilizopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambazo thamani yake ni takriban shilingi milioni 70.

DSC_1824

off12-600x600

5. Gharama anayotumia kuwatunza mbwa wake, Vanny na Gucci

Mtandao wa Global Publisher jana uliandika, “KWA wale wenye hali ngumu kimaisha wataishia kusema; ni kufuru iliyoje kwani staa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu hivi karibuni amewafanyia mbwa wake wawili ‘shopping’ iliyogharimu dola 4,000 za Kimarekani (zaidi ya Sh. milioni 6.5 za madafu).

Wema aliteketeza kiasi hicho cha fedha kwa kuwanunulia mbwa hao pafyumu, viatu na nguo, alivyoagiza kutoka nchini China, lengo likiwa ni kuhakikisha wanaishi katika mazingira mazuri.

Akizungumzia ‘shopping’ hiyo nyumbani kwake Kijitonyama, jijini Dar, Wema alisema: “Kiukweli nawapenda sana hawa mbwa, ukinipasua roho yangu utawakuta ndiyo maana nataka wavae na kunukia vizuri, kinyume chake siwezi kuwa na amani.

0caeb4ac921811e28e6622000a9f0a1a_7

Vanny na Gucci wakicheza
Vanny na Gucci wakicheza

83b019e2914b11e28e0922000a9f1335_7

818e18e0921c11e2af9022000a1f9a23_7

90197700921811e2996f22000a1fbc6f_7

Vanny
Vanny
Vanny
Vanny
Gucci akiwa amelala
Gucci akiwa amelala
“Najua watu wanaweza kushangazwa na kitendo cha mimi kutumia kiasi hicho cha fedha lakini sioni kama ni tatizo kwani ni kitu ambacho kinanipa furaha katika maisha yangu.”

Leo kupitia Instagram, Wema ameandika, “Vanny ake heading to da hospital…. my poor baby is sick…. nat happy at all, hope u get better soon.”

6. Shilingi milioni 13 alizomtolea Kajala baada ya kusomwa hukumu yake

Jana Wema Sepetu alimake headlines baada ya kutoa mfukoni mwake shilingi milioni 13 kulipa faini aliyopigwa muigizaji mwenzie Kajala Masanja aliyehukumiwa jana kwenda jela miaka mitano ama kulipa kiasi hicho cha fedha.

Akizungumza exclusively na Bongo5, Wema amesema hakufikiria mara mbili kutoa kiasi hicho cha fedha.

“Kusema kweli wanasemaga kwamba kutoa ni moyo so naamini what I did is best, nimetoa kwasababu I had to do it and sikuthink twice kuhusu kufanya hivyo,” amesema Wema.

“Nimefanya kama namsaidia rafiki yangu kama namsaidia ndugu yangu na sidhani kama ingekuwa ni kitu kizuri kumuona mwenzako anaingia kwenye dhahama, kwenye tabu, kwenye mateso na wakati nina uwezo wa kumsaidia kwahiyo I just did what I had to do.”

7. Jinsi anavyomwaga hela kwenye sherehe mbalimbali

Katika katika sherehe za 8020 Fashion’s Women Celebration zilizofanyika kwenye siku ya wanawake duniani, Wema aliuteka ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya kumwaga mihela kwa mwimbaji maarufu wa Taarabu nchini, Khadija Omar Kopa. Wema alimwaga mkwanja huo kumpongeza Khadija kwa kukonga moyo wake.

Hayo ni machache tu tunayofahamu na kwa hesabu hizo, bila shaka utakubaliana nasi kuwa Wema Sepetu ana mkwanja mrefu!!!

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW