Burudani ya Michezo Live

Exclusive: Diamond na Wema walikutana Hong Kong, bado ni wapenzi na wala hawafanyi movie

Kuna sababu zaidi ya 100 kuwa ‘ile inayoitwa’ movie ya Diamond na Wema Sepetu iliyopewa jina na Diamond, ‘Temptations’ haipo na kama unaingoja, utaingoja hadi miguu iingie tumboni. Hakuna movie.

IMG-20131009-WA0007

Diamond na Wema Sepetu walikuwa wakila bata na kufurahia kama wapenzi wengine wanaopendana kwa dhati. Kwa kuangalia picha tu, ni rahisi mno kujua penzi zito kati ya wawili hawa. Picha hizo ni ishara kuwa, Diamond na Wema hawajawahi kuachana na Diamond amekuwa akimcheat mpenzi wake Penny.

Wazungu wanasema, kama hujafanya utafiti hauna haki ya kuzungumza, hivyo ili kuonesha kuwa hizi si brabra tu, tumefanya utafiti kwanza.

IMG-20131009-WA0008
Wema, Diamond na binamu yake Romeo wakiwa Hong Kong

Ukweli wa kwanza tulioubaini ni kuwa, Diamond na Wema Sepetu walikutana Hong Kong na sio Malaysia. Wema alienda huko takriban wiki tatu zilizopita na hivyo Diamond alimfuata baada ya kumaliza show yake ya Malaysia. Kwa mujibu wa msichana aitwaye Alice aliyeiambia Bongo5, Diamond alisafiri kutoka Kuala Lumpur, Malaysia kwenda Hong Kong kumfuata Wema kwa ndege ya kampuni ya Air Asia.

“Nilipanda na Diamond flight moja from KUL to HKG tena ilikua ni Air Asia X flight number 567 alipandia KUL-LCC Terminal nilimuona kwenye lounge direct nikashangaa anafanya nini huku na baada kufika HKG sijui hata alipotelea wapi kumbe haya yote ndo alikua akiyafuata hongera zao,” alisema Alice.

Huko, Diamond na Wema wamekaa wote kwenye hoteli moja na mpenzi wake Penny hakuwa anajua kuhusu hili hadi picha hizi zilipoanza kuenea na yeye ameshtuka kama walivyoshtuka wengine.

Haijajulikana picha hizo zimesambazwa na nani lakini kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, kuna uwezekano kuwa picha hizo zimesambazwa na Wema wenyewe kwa kusudi la kumuumiza Penny. Kuna taarifa zimeifikia Bongo5 kuwa, Penny ameumizwa mno na picha hizo na amekuwa akilia siku nzima. Hata hivyo binafsi hatujaweza kuthibitisha taarifa hizo.

Jitihada za kumtafuta Penny azungumzie suala hili zimegonga mwamba kwakuwa simu yake haipokelewi.

18594b3a2d2e11e3bfc922000a9e08f9_7
Penny

Hivi karibu kwenye birthday ya Diamond, Penny alielezea kuwa uhusiano wake na Diamond ndio mgumu zaidi katika mahusiano yote aliyowahi kuwa nayo.

“Not the easiest relationship I’ve ever had..but its the most intresting! When I’m down, he would make me feel on top of the world, my bestfriend, my brother, my soulmate, my baby, my man. My strength, my joy, my love, Ohhh!!! What else do I gotta say? I love u, and its been a blessing to have met you, u taught me that love is just Me&You the rest shouldnt matter or make me loose my sleep, today I ask God to bless u a million more times, the sweetest boyfriend ever!!! Crazie too..unpredictable mind, through the ups and downs Im gona hold you down til God says so..you have taught me that love conquers all, that Love is pain, but the pain is worth the while..I love you baby,” aliandika Penny.

Miaka ya nyuma, Wema na Penny walikuwa marafiki wakubwa lakini kwa mujibu wao wenyewe, urafiki wao uliharibika hata kabla ya wote kufahamiana na Diamond.

“Urafiki hatuna,” Penny aliliambia jarida la Mzuka kwenye makala ambayo haikuwa kutoka. “Mimi sidhani kama nina uadui naye personally, sijui yeye na urafiki hatuna. Let me just say kwamba sio kwasababu ya Diamond. Nadhani mimi na yeye tulikuwa tuna issue zetu nyuma ambazo hazikuwa resolved so tulikuwa tuna distance mimi na yeye. Tulikuwa hatuongei maybe kwa mwaka labda kama sio miezi nane, we had our own issues kwahiyo hatukuwa marafiki vile tena kama tulivyokuwa zamani. So mimi kuwa na uadui naye sidhani kama nina uadui. Mimi am happy unajua, mimi ndo hivyo mimi naishi maisha yangu am happy na nilichonacho am happy with my man, am happy na watu wangu so am good mimi sina tatizo naye kabisa.”

Naye Wema kwenye interview na Mzuka aliwahi kuzungumzia alivyojiskia Diamond kuwa na uhusiano na Penny, rafiki yake wa zamani.

“It’s a free world, kila mmoja ana uhuru wake wa kuishi anavyotaka yeye. They met, they fall in love wameanza mapenzi, mtu yoyote anaweza kufall in love na mtu yeyote asiwe questioned. Love doesn’t ask why, haiulizi kwanini, because alikuwa rafiki yangu then I can’t NO. Wapendana, I wish them all the best. Mimi na Penny si kwamba hatuongei sio sababu ya hii issue, tuna drama zetu tu za huko nyuma kwahiyo hii issue ni muendelezo tu,” alisema.

Ikumbukwe kuwa, Wema na Diamond waliwahi kuingia kwenye ‘kile kilichoonekana’ kama ugomvi mzito, baada ya Diamond kumrekodi mpenzi wake huyo wa zamani alipompigia na kuisambaza sauti kwenye vyombo vya habari.

“Sikuwahi kudhani kwamba Naseeb ni mtu wa aina hiyo kufanya kitu alichokifanya. Though nimesema kwamba nitaacha kama ilivyo na nisingependa kuiongolea lakini nilikuwa very disappointed, very very disappointed,” Wema aliliambia Mzuka.

Tunasubiria kushuhudia muendelezo wa drama hii kutoka kwa Malkia na Mfalme wa drama Tanzania.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW