Burudani

Exclusive: Director Nisher afunguka mengi kuhusu ukimya wake na changamoto alizopata mwaka huu

Mshindi wa tuzo ya Muongozaji Wa Video Anayependwa katika Tuzo Za Watu 2014, director Nisher amefunguka kwa kirefu mambo mbalimbali kuhusu ukimya wake.

nisher intro

Muongozaji huyo wa video za muziki kutoka Arusha aliyekuja kwa kasi na kuwa gumzo kutokana na video kali alizotoa kuleta ushindani, amepiga story na Bongo5 na kuzungumzia mambo yaliyosababisha ukimya wake pamoja na changamoto alizokutana nazo mwaka huu.

2014 ni mwaka ambao ulifanya vizuri sana ikiwa ni pamoja na kushinda Tuzo Za Watu, na matarajio ya wengi yalikuwa kwamba 2015 ungekuwa mwaka wa mapinduzi zaidi kwako, Nini kimebadilisha mambo na kuwa tofauti na matarajio kwa kufanya video tatu tu hadi sasa (Bongo Hip Hop – Fid Q, Young Suma – Hatujivungi, Killy – Rudi)?

Nisher: 2012/2013/2014 pengine ni miaka ya kihistoria kwangu kama “director” wa music videos nchini kwa sababu mimi nilikuja Katika kipindi cha Adam Juma na John Kallage, hao ndio walio kua ma-director wakubwa wakati huo wenye kazi zenye ubora, na wasanii wa nchini hawakua wakitafuta kwenda international kivile, walikua akitafuta videos KALI na ideas tofauti, so kwangu ilikua advantage kuja kufanya revolution ya videos kali which hiyo Kila mtu anajua kua ilikua kazi yangu! Malengo yangu hayakua mashindano, sikuja kutafuta mashindano, nilikuja kutafuta jina/platform ilikuweza kuendeleza talents zangu nyinginezo ikiwemo Music production na Films.

Nilipotua kwenye industry watu walinikimbilia zaidi sababu nilikua “Option Mpya”….. that’s how This Business works, kukiwa na options watu wanapenda kuzitumia, miaka hiyo watu walinifaidi zaidi kutokana na ukweli kwamba hapakua na mtu mwingine aliyefanya videos nilizofanya kwa ubora ule nilio ufanya kwa miaka hiyo!

Nisher tuzo

Baada ya kuanza kushine na jina kukua ulikutana na changamoto gani?

Nisher: Nilikutana na challenge mbali mbali moja wapo iliyokua kubwa zaidi mbali na kupishana ideas za video na wasanii ni usambazaji wa videos, hapo ndipo game ilipo change, wasanii hawakutaka tena kuona videos zao ITV, TBC, STAR TV, CHANNEL 10, EATV na CLOUDS TV peke yake, walitaka kuanza kuvuka border, so ikabidi nianze kutafuta connections…. Which tunakuja kuona msanii kama Ben Pol aliweza kua na video namba moja nchini #Jikubali na video hiyo kupigwa #Channel-O mwaka mzima hii ikiwa ni video yake ya kwanza kuvuka nje ya nchi na video ya kwanza ya Ben Pol kupata Views nyingi YouTube mwaka ule!! Video zingine kua kama Kijukuu ya Young dee, Baby ya Mirror, Bila Wewe ya Jordan, Nje Ya Box Video ya Weusi yao ya kwanza Kuvunja record ya VIEWS 20,000 Ndani ya Siku 1 na kuvuka Kwenda channel za kimataifa kama Channel O (kwa mwaka mzima) , Trace kuicheza wiki ya kwanza na MTV kuicheza siku tatu baada ya Kutoka mwaka ule, Ilikua Big Deal kwenye industry na Landmark kwangu kama Director!!! Videos zilifuata nyingi sana kuchezwa nje ya nchi list ni ndefu, kwa director yeyote wa sasa hivi level hiyo ni level ya juu sana Katika career!!

2014 Kwangu Kuwa Director namba 1 nchini kuwahi kushinda Tuzo Ni kitu cha kihistoria Sana kwangu na Game nzima la Video Directors Tanzania!….. Ikumbukwe kua hapakuwahi kua na tuzo zozote za Ma-director nchi hii so kwangu kuufungua huo ukurasa itakumbukwa daima Milele!!!

nisher location

Unauzungumziaje mwaka 2015 kwako kwasababu umefanya video chache tofauti na matarajio ya wengi waliodhani baada ya kushinda tuzo ungefanya makubwa zaidi

Nisher: Mwaka 2015 nilijua utakua na changamoto zaidi sababu options (ma-director) zimekua nyingi zaidi na wasanii walishaanza kutaka kuonekana zaidi Afrika badala ya East Africa tu, so Kukatokea MASHINDANO ambayo ndio yanayoendelea mpaka sasa, ikapelekea safari za wasanii nje ya TZ kua nyingi, hii ikalazimu Directors wote wa nyumbani kushusha bei za video ili wasikose wateja, kitu ambacho kwa directors wakubwa ni mmomonyoko wa biashara sababu kushuka kwa bei inamaanisha huwezi fanya kazi kubwa kwa budget kubwa kama zamani na huwezi kufanya usambazaji kwenye TV stations za nje sababu hizo process zinataka fedha za ufuatiliaji!!!

So wasanii wengi Wa class A nchini wote waliona ni bora kufanya kazi nje kuliko ndani sababu nje watalipa hela ya video na hiyo hiyo itasambaza kazi kuliko kutulipa sisi wa nyumbani wakisahau kua wanatumia nauli za ndege na hela za hotels ambazo wangeweza kusave wakafanya kazi bora tu nyumbani!!!

Kitu nimejifunza ni kwamba wasanii wengi husema directors wa nyumbani wasumbufu na hawathamini kazi za wasanii, hili pengine likiwa ni kweli na sio kweli maana binafsi nadhani ni kuutambua wakati tu na kujua kua hii ni biashara! Huu Ni wakati wa Tanzania kushine, na kwenda international zaidi, ila kama budget haziruhusi mtu kama mimi siwezi kujikaza ili niwe na video Kwenye market ili nipate attention wakati HAINILIPI, bora nifanye kazi zingine kwanza then wasanii wakija kuona wanatumia hela sana nje wakaamua kurudisha nguvu nyumbani ni rahisi kurejea!!! Ila haya mashindano wanayoyafanya Kumuiga Diamond kua kama yeye watayafanya mwishowe watachoka….. Kila mtu ana nyota yake kwenye hii industry…. Huwezi Fanya hii biashara kwakuiga flani anafanya nini na wewe ndo ufanye utafika mahali utachoka na hela haitakuruhusu!!!!

Nisher studio

Kwa muda huu uliokaa kimya ni kitu gani unajishughulisha nacho mbali na kushoot video? Na ukimya huu hauoni kama unaweza kuwa na athari kutokana na ukweli kwamba kadri unavyoendelea kuwa kimya ndio unavyozidi kupotea?

Nisher: Kwangu sioni vibaya kutulia na kuja kurudi when I feel the time is right, jina langu ni kubwa tayari ni kama ndege yenye mafuta inasubiri mvua mbaya ziishe inyanyuke!!!

Sasa hivi nafanya biashara zangu Arusha, including music production, mwaka huu nime produce kazi ya Fid Q ya ‘Bendera ya chuma’ ambayo aliiperform live at #Cockestudioafrica, which hiyo was a big deal for me, Kuna baadhi ya wasanii wananicheki kufanya kazi za video ila changamoto kwao inakuja kwenye swala la hela, wakati wa malipo wanapotea, sitataja majina ila ni wasanii wakubwa tu!

Kazi ya kuongoza video imeshakutengenezea pesa kiasi gani toka uanze?

Nisher: Kiukweli through out my career kama director na music producer na kazi zangu mbali mbali nje ya hizi fani nimetengeneza hela nyingi ambayo nikisema sasa hivi nisifanye hii kazi tena bado nitakua fine kabisa!!… This is why hata ninapopewa deal ya kazi napenda kuifanya nikiwa comfortable na client wangu aridhike na kazi yake kwa asilimia 1000/100….. sitaki kufanyia njaa tena!!!

Ikiwa tunaelekea kuumaliza mwaka 2015 una waahidi nini mashabiki wako kwa mwaka ujao?

Nisher: 2016 siwezi yasema ya Mungu, mimi napanga Mungu anapanga pia… Ila ninachojua for now I’m in a peaceful place in life, Sihitaji kumfurahisha mtu yeyote duniani… Nimeishi maisha yangu miaka yote nikipendeza watu tu nikasahau kujifanyia mema mwenyewe so kwasasa najitendea wema kwanza!!!

Kitu kimoja ninacho waahidi Mashabiki wangu wale waukweli sio wale wakupita Ni kwamba Nitarudi tena na Nitawafurahisha Zaidi kuliko hata mwanzo, isipokua wawe na subira tu, Movie kali haitaki haraka!!!!

NISHER WILL BE BACK, WHEN READY!!!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents