Habari

Exclusive: G-Nako aelezea sababu za Ben Pol kutosikika kwenye wimbo wake mpya ‘Wara Wara na Mpira’ licha ya kusikika kwenye Teaser

Jana mweusi G-Nako a.k.a Wara Wara aliachia wimbo wake mpya “Wara wara na Mpira”, ikiwa ni siku kadhaa toka atoe teaser ya wimbo huo . Inawezekana wewe ni kati ya watu walioisikia teaser, na kama ndivyo lazima utakuwa unajiuliza kulikoni mkali wa R&B Ben Pol aliyesikika katika teaser ya wimbo huo hajasikika katika wimbo uliotoka na badala yake amesikika msanii mwingine kabisa aitwaye ‘Henry’.

Gnako

G-Nako amezungumza na Bongo5 leo na kuelezea sababu za kutosika Ben Pol kwenye wimbo huo kama ilivyokuwa awali.

“Unajua Idea ilipotoka Arusha kuja kwa Chizan Brain ilibadilika, mahadhi yakabadilika na mdundo wenyewe uka-change kidogo na Henry alipofika akaongezea base line na piano inayosikika pale, mimi pia ikabidi niingize mistari yangu upya, Henry alikuwepo na akafanya kitu kizuri. “Lakini pia kabla ya hapo Ben Pol nilikuwa nimeshawasiliana nae, lakini kutokana na kuwa na kazi nyingi, alikuwa busy sana ikabidi nimuache tu aendelee na shughuli halafu Henry amalize tu ile kazi pale kwa sababu wimbo ulikuwa unatakiwa utoke.”

Akimzungumzia Henry ambae ni msanii mpya kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, mkali huyo wa ‘Mama Yeyo’ amesema jamaa ni msanii mwenye uwezo mkubwa na kwamba ameshawahi kutoa wimbo lakini haukufanya vizuri, na hivi karibuni anatarajia kuachia wimbo mpya ambao G-Nako ameusifia.

“Henry ni jamaa mmoja mbaya sana, anaimba sana, anauwezo wa kupiga vyombo vingi vya muziki pia. Baada ya wiki ataachia wimbo wake mpya ni mzuri sana kwa kuwa mimi nimeshausikiliza.” Amesema G-Nako

Kama hujapata nafasi ya kuusikiliza wimbo mpya wa G-Nako usikilize hapo chini “Wara wara na Mpira”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents