Burudani

Exclusive: Gadner azijibu tuhuma za Lady Jaydee (Video)

Kwa mujibu wa Lady Jaydee, Gadner G Habash alikuwa ni mume aliyekuwa akimdhalilisha kwa kutongoza wanawake mbele yake.

Jaydee aliyaanika hayo kwenye Instagram March 20. Hata hivyo hadi Ijumaa, Gadner alikuwa hajawahi kuzijibu tuhuma hizo.

“Kwa sasa hivi kusema ukweli nimetajihidi na mara nyingi napendelea kutozungumza sana uhusiano wangu uliopita kwasababu nina hofu kwamba nitamnyima mwenzangu uhuru wa mambo yake binafsi,” Gadner aliiambia Bongo5.

“Kwahiyo naepuka kuzungumzia hiki kitu, kinaleta amani zaidi.”

“Kwakweli sijui ni nini ambacho mimi nimetuhumiwa, nasikia tu ila namshukuru Mungu na nasamehe kila kitu na natakia heri kila kitu kiende sawa,” aliongeza.

Gadner alisema tayari amesonga mbele na maisha mengine.

“Kwasababu mimi ni mtoto wa kiume, siwezi kukaa na upweke na Mungu hajatuumba hivyo. Kwahiyo kusema kama nina mahusiano mengine siwezi kukataa yapo, isipokuwa sio kitu ambacho naweza kukiweka hadharani.”

Bado mtangazaji huyo wa EFM ana imani katika ndoa ingawa anadai hawezi kukurupuka.

“Kuoa ni jambo la baraka huwezi kupanga tu ghafla kama hivi kwahiyo itakapotokea kama Mungu amependa basi heri, kama itakuwa haijatokea, wapo wengi pia wanaishi bila kuoa na wako sawa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents