Habari

Exclusive: Grace Matata azungumza kuhusu uzazi, muziki, kazi, Mlab, collabo na Jide (Audio)

Jumamosi ya July 27 kwenye Kilinge cha Msasani Club jijini Dar es Salaam, tulipata fursa ya kuzungumza na muimbaji mahiri wa kike nchini, Grace Matata.

Grace Frontcover2

Kwenye mazungumzo hayo, Grace ambaye ni mama wa mtoto wa kike mwenye miezi 11 sasa, Ella amezungumza kuhusu maisha yalivyobadilika baada ya kuwa mama, kazi anayofanya zaidi ya muziki, collabo na Lady Jaydee, studio iliyomtoa kimuziki Mlab, wanamuziki anaopenda kufanya nao kazi na muziki anaopenda kusikiliza.

Kuhusu maisha yalivyobadilika baada ya kuwa mama

Inafanya malengo yako yabadilike priority zako zinabadilika kabisa. Miezi 10 na something iliyopita nilikuwa nawaza tofauti sana but dakika ile unapata mtoto unatakiwa ujielewe sababu ni maisha umekabidhiwa, if you mess up, you mess her up, kwahiyo it changes everything. Mwanzo unaogopa, baadaye unajifunza, baadaye unagundua kwamba ni blessing, it’s a blessing every day.

Anachofanya kwa sasa tofauti na muziki

Right now nafanya kazi na kampuni moja wanaforward mizigo lakini soon ntaanza kufanya kazi na shipping line

Annete 1

Kuhusu ukimya wake kwenye muziki

Nadhani nilipojifungua mpaka a few months mpaka mwezi wa tano nilikuwa nipo kimya sana sababu nilikuwa nimebase zaidi kwenye mtoto lakini recently kazi zinaendelea kama kawaida.

Kuhusu kama bado yupo MLAB

MLAB na mimi mkataba wetu umefika mahali umeisha lakini MLAB walitengeneza ile brand ya Grace Matata wakanisaidia nilipokuwa najaribu kutengeneza sound yangu kwahiyo walinisaidia kukua na wamenifisha hapa, siwezi kusema siko MLAB tena na siwezi kufanya nao kazi tena, NO. But unavyozidi kwenda mbele unagundua kwamba inabidi ufanye vitu vingine tofauti tofauti, ufanye kazi na watu wengine tofauti. Kwahiyo this time around nataka kufanya kazi na watu tofauti.

Kuhusu kufanya collabo na Lady Jaydee

Tunaiongela mara nyingi sema Jaydee mambo mengi sasa hivi yamembana, ana tour, ana nini, hajatulia sana na mimi pia this time nimehama kazi, nimetoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwahiyo mambo yakawa ni mengi sana lakini every day hakuna siku tunayokutana hatuongelei hilo suala.

11

Kuhusu wasanii anaotaka kufanya nao kazi

East Africa, Collo, nampenda kweli Collo kwa rappers. Kwa waimbaji nampenda sana Juliana. Kwa Tanzania Karola na Jaydee ofcourse.

Kuhusu muziki anaosikiliza

Kwa Tanzania nampenda Ali Kiba, hakuna kitu ambacho amewahi kuimba sijakipenda. Akina Ommy Dimpoz nawasikiliza. Kwa hip hop akina Stereo, One, akina Nikki. Kwa nje napenda sana wanawake wanaopiga live instruments, wanaopiga kama gitaa au piano.

Sikiliza Interview yote hapa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents