Tia Kitu. Pata Vituuz!

Exclusive: Hussein Machozi asaini mkataba na Candy n Candy ya Kenya, msikilize akiuzungumzia

Hussein Machozi atakuwa chini ya usimamizi wa kampuni mpya ya nchini Kenya iitwayo Candy n Candy ambayo pia imemsainisha Mr Nice. Akiongea na Bongo5 Machozi amesema mkataba huo umekuja wakati muafaka kwakuwa kwa muda mrefu alikuwa anatamani kuwa chini ya menejimenti ya uhakika.

531737_4271976050030_1492809986_n

“Wenyewe watasimamia kazi zangu zote kiujumla kulingana kwa chochote kinachoingia kwa Machozi,” amesema.

“Jamaa watanifanyia kila kitu kuhusiana na studio, sehemu ya kukaa, usafiri. Jamaa tumesaini kwa muda wa miaka mitatu. Siku nyingi sana nilikuwa natafuta mtu wa kuwa karibu na mimi ilikuwa ngumu sana lakini namshukuru Mungu jamaa wamepatikana na wako serious na mimi naamini tutafanya kazi.”

Machozi amesema licha ya kuwa na uwezo mkubwa anashangaa jinsi baadhi ya wadau wa muziki nchini wanavyomchukulia poa hadi watu wengine tofauti wamesafiri kutoka Kenya kuja kumpa mkataba mzuri.

“Kila mtu ambaye nimekuwa nikimjaribu tufanye kazi watu wanakuwa wazito. Mara nyingi huwa inaniwia vigumu kwamba labda watu hawanithamini kwasababu siwezi ama? Kwakweli mawazo yangu kibongobongo yalikuwa yameshaondoka. Ukiangalia kuna wasanii wengi ambao walikuwa na mawazo yao kibongobongo na wamekishwa, tuko nao madereva wa bajaj sasa hivi sasa sitaki hiyo hali inikute mimi. Inaniuma sana kuona watu wa nyumbani kwangu wananichukulia poa halafu watu wa nchi jirani wananikubali, inauma sana.”

Ameongeza kuwa anatarajia kuripoti Candy n Candy jijini Nairobi baada ya mwezi wa Ramadhan.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW