Burudani ya Michezo Live

Exclusive Interview: Baba Levo adai kuwa Diamond ametumia kionjo cha wimbo aliotaka kumshirikisha katika chorus ya ‘My Number 1’ (Audio)

Idadi ya wasanii wanaodai kuumizwa na ujio wa single mpya ya Diamond Platnumz ‘My Number One’ inazidi kuongezeka, baada ya Dayna ambaye tulizungumza naye kwa kirefu jana, Baba Levo naye jana ametoa kilio chake na kudai kuzungukwa na Platnumz.

levo

Baba Levo na Diamond wako katika kampuni moja ya Leka Dutigite, na pia ni wasanii wanaowakilisha mkoa mmoja wa Kigoma, lakini pamoja na hayo Baba Levo jana (September 4) kupitia ukurasa wake wa facebook aliwasilisha malalamiko yake kwa mashabiki:

“ZAMANI nilikuwa nikiskia mtu analalamika kaibiwa wimbo au kaibiwa njia. Nilikuwa naona ni kama maigizo na mtu kutafuta kick ya kupandia .ila leo nasema wazi DAIMOND PLATNUM amechukua korasi ya wimbo wangu niliopanga kufanyanae unaitwa SWEATY SWEATY na kuiimba kwenye wimbo wake mpya NO 1 .. kanizungusha sana kumbe alikuwa na lengo lake…ila baridaa maisha yanasonga…”

Bongo 5 ilimtafuta Baba Levo kutaka kujua undani wa swala hili sababu imekuwa ghafla tofauti na Dayna ambaye alianza kulalamika kwenye mitandao hata kabla ya video ya Diamond kuzinduliwa wala kutoka. Baba Levo anadai kuwa Platnumz ametumia kionjo kilichokuwa katika kiitikio cha wimbo wake aliotaka kumshirikisha.

Baba Levo amesema kuwa zaidi ya miezi sita iliyopita alimtafuta Diamond ili amshirikishe kwenye wimbo wake unaoitwa Sweety Sweety,
“ Diamond nikamwambia bana nina wimbo wangu hivi na hivi nataka kufanya na wewe akaniambia hamna shida wewe fanya ya kwako halafu mi niachie nini nafasi yangu and then tutakuja tufanye nini tufanye kwasababu wote ni ndugu Leka dutigite na vitu ka izo”.

“Nilipomaliza kuandika nikamwambia mi bana nimeshamaliza kuandika na kila kitu, akaniambia niimbie nikamwimbiaaa, akaniambia itabidi uniletee demo kwani umefanyia wapi huo wimbo, nikamwambia mimi nimefanyia kwa nani kwa mo fire, au sio bana, akaniuliza Mo fire ndo nani nikamwambia producer wangu alietengeneza Yalayala, akasema aah kati ya vitu vinavyokufelisha baba Levo ni kufanya kwenye production ndogo na vitu ka izo nini na nini, inabidi utafute production ambayo ni kubwa kidogo”.

Baba Levo akaendelea kusema kuwa aliufata ushauri aliopewa na Platnumz na kuamua kuihamishia kazi hiyo kwenye studio nyingine.

Baba Levo amesema kuwa alianza kupata taarifa juu ya wimbo wa Diamond kutoka kwa mshikaji wake aliyedai kausikia wimbo wa My Number 1 kwa wanafunzi wa IFM kabla video haijatoka ndipo akamuuliza mbona ametumia kionjo cha wimbo wake anaotegemea kutoa..

“kilichokuja kufanyika, kanizungusha zungushaa badae nikaja nikaambiwa kuna mtu akaniambia ebana eh Levo eeh, sababu mimi unajua mimi mtu wa maskani nikikaa na wana nini naimba ili niskie maoni yao, unajua kawaida ya Diamond huwa anavujisha kwanza nyimbo zake anavujisha ikishavuja then anaskia watu wanasemaje, akanimabia kuna wimbo mmoja nimeskia IFM wa diamond ameimba vile vile kama chorus ile ile ya kwako. Nikamwambia ah mimi mbona sijaskia wimbo nikafatiliaaa nikashindwa kuupata huo wimbo”

Levo kaendelea kusema watu waliendelea kumpigia simu akiwemo H Mbizo ambaye pia alimwambia kitu hicho hicho kuwa ameusikia pia wimbo wa Diamond wenye kionjo cha wimbo wake, lakini Levo alijitahidi kujizuia kusema chochote mpaka atakapokuja kuusikia wimbo wa Diamond na pia asingeweza kulalamika kwa wimbo ambao hata mhusika hajautoa rasmi.

Baba Levo anadai hata wakati Diamond anazindua video yake wiki iliyopita yeye alikuwa hajabahatika kuusikia licha ya kusikia Dayna akilalamika kuibiwa beat ya wimbo huo huo mpaka jana asubuhi ndio amefanikiwa kuiona video hiyo na kuthibitisha kile alichokuwa akiambiwa na watu.

Muda mfupi uliopita Baba Levo amesisitiza kupita ukurasa wake wa facebook kuwa Diamond amecopy chorus ya wimbo wake na hatafuti ‘kick’

“NARUDIA tena nina asilimia 100 DAIMOND PLATNUM amecopy KORAS yangu coz nimekuwa nikimuimbia kila tunapokutana kwa lengo la kumshirikisha kwenye wimbo wangu (SWEATY SWEATY) ni zaidi ya miezi saba au nane imepita akinizungusha tu. na kwa kudhibitisha Hilo mimi nina DEMO 5 za KORASI yangu ambazo nimefanya kwenye studio mbali mbali Ya kwanza 1 kwa MORE FIRE magomeni 2 STUDIO SINZA 3 kwa TUDY THOMAS mbezi 4 kwa G BAKUZA KIGOMA 5 kwa MR T TOUCH mwenge… “Ninaweza kuwasikilizisha watu demo zote Tano lakini sio kuuachia huo wimbo coz ntaonekana walewale wategemea KICK. wakati MIMI KWA SASA sihitaji kick ya mtu coz msimu huu nina nguvu ya kutosha. na nina jiamini.. ukitaka kuamini angalia kilichotokea FIESTA MTWARA JUZI..”

Msikilize hapa
[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/108948824″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Sikiliza demo ya Baba Levo

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/108950537″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW