Burudani ya Michezo Live

Exclusive: Interview na host wa KTMA 2013 Tahjir Siu aka TJ wa Magic FM/Channel10

Tahjir Siu aka TJ ni mtangazaji wa kipindi cha Daladala Beatz cha Magic FM na pia hutangaza kwenye kituo cha runinga cha Channel 10. Ni mtangazaji mwenye uwezo mkubwa na uelewa wa kutosha kwenye masuala ya burudani.

IMG_3144
TJ kwenye KTMA 2013

Pengine ndio sababu iliyowashawishi waandaji wa Kilimanjaro Tanzania Music Awards mwaka huu kumfanya mmoja wa hosts wa tuzo hizo. TJ ambaye kwake KTMAs ndio ilikuwa show ya kwanza kubwa kuhost katika career yake, alionekana kumudu vyema kazi yake na kuyavutia masikio na macho ya watazamaji wengi usiku huo.

BB3SbDuCQAA8bf8

Akishirikiana vyema na host mwenzake, Zembwela, mara zote TJ alionekana kujiamini kama host mkongwe. Sauti yake tamu na yenye mamlaka ilikuwa ni sababu moja kubwa ya kwanini KTMA imefanikiwa sana mwaka huu.

BMYzNI7CIAEqE5u

A9-G_1OCcAAE-kR

“This one was such a big opportunity kwangu na ilikuwa kubwa sana as you know KTMA is a big event, kwahiyo kilikuwa ni kitu kikubwa sana kwangu,” amesema Tahjir.

BMY0PkdCMAEVjft

“Nisingeweza kufanya bila watu waliokuwa wamenisimamia nyuma at the whole KTMA crew, walikuwa wananiencourage kwenye kila kitu. Sikutegemea kwamba wangeweza kuniamini kwamba naweza kufanya kitu kikubwa kama kile lakini kwa uwezo wao pia kunipush mimi nimeweza kufanya kazi nzuri.”

BAwbjeQCUAAeszi

TJ amesema amepokea pongezi nyingi mno kutoka kwa watu mbalimbali nchini wakiwemo waandaji wa tuzo hizo.

“Mr George Kavishe alikuja kwangu akaniambia ‘TJ you did a spectacular job, thank you very much kwa kutufanya tuendelee kuwa mbele with what you did’ that was one of the greatest congratulations ambazo nimepata,” amesema TJ.

TJ amesema pongezi nyingine kubwa ni kutoka kwa baba yake mzazi ambaye hakuwa anajua kuwa aliiangalia show hiyo live kwenye TV nyumbani.

“I wasn’t expecting that kutoka kwa baba yangu, baba yangu ni mtu wa dini sana. When he said ‘hongera, I am proud of you’ it’s one of the things that completed everything.”

A__oDxCCIAEBsh4

Mtangazaji wa kipindi cha XXL cha Clouds FM, B12 hakuficha hisia zake kuhusiana na kazi nzuri ya TJ kwenye jukwaa na aliamua kumpongeza wakati ameitwa kumtangaza mshindi wa mtunzi bora wa mashairi ya Bongo Flava iliyoenda kwa Ben Pol.

“I like B12, napenda utangazaji wake, I like what he does, kwahiyo If I get to work with better people, fresh kwangu,” alisema TJ kujibu swali kama alimsikia B12 akimpa pongezi siku hiyo.

Msikilize zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW