Burudani ya Michezo Live

Exclusive Interview: Rama D afunguka kuhusu surprise alizozikuta TZ, uhusiano na Sugu, Kili, Prof J, Jaydee

Mwanamuziki wa R&B Rama D amerejea nyumbani Tanzania baada ya kukaa kwa mwaka mzima nchini Australia ambako ana familia huko. Amezungumza na Bongo5 kwenye interview exclusive kuhusu surprise alizozikuta kwenye muziki wa Bongo, uhusiano wake na Sugu baada ya harakati za Antivirus kuisha, harakati za sasa za Lady Jaydee, Kili Music Awards, jinsi anavyouchukulia muziki wa sasa wa Profesa Jay na kuhusu anachofanya nchini Australia.

535661_594201670609340_1088683190_n

Kuhusu surprise alizozikuta

Kitu ambacho kimenisurprise sasa hivi ni kuona maadui wanarudi nyuma, yaani yale mashambulizi ambayo tulikuwa tunayafanya naona wanazidi kurudi nyuma. Sasa hivi inatakiwa iongezwe nguvu kwa sisi wasanii yaani kushikana kidogo tu halafu tuweze kuwapush kwenye mifereji ya maji waende mbali. Kitu kingine naona kitu ambacho nilikuwa nakipigania siku nyingi sana. Nilikuwa napigania sana muziki wa RnB halafu sasa hivi naona unapata nafasi, yaani kuna watu wanapewa nafasi kama hawa akina Ben Pol, akina Steve RnB, Belle 9. Sababu kuna propaganda ambazo zilikuwepo, mtu akifanya RnB anaambiwa labda fanya kiduku ndio utauza so unawadisappoint mashabiki wako waliokupokea mwanzo.

Kuhusu kumalizika kwa antivirus na uhusiano wake na Sugu

Uhusiano wangu na Sugu ni mzuri hauna matatizo kwasababu nilikuja kufanya research nikagundua kwamba siasa ni mchezo mchafu sana na hii siasa ndio inawafanya mpaka washkaji wakabadilika. Unaweza kuwa unafanya harakati upo frontline lakini end of the day na wanasiasa ni rahisi sana kukaa chini na kukutuliza. Mimi (Sugu) namlaumu kitu kimoja aliangalia maslahi yake kuliko maslahi ya watu wengine. Lakini kitu ambacho nataka kuwaambia ni kwamba Sugu kama Sugu hakufanya kazi ambayo sisi tuliifanya sisi tulifanya movement kubwa sana mpaka kuifikisha movement hapo ilipofika.

Kuhusu harakati za Jaydee

Anachokiongea ni kitu ambacho sisi tayari tulishakiongea kwahiyo yeye anachofanya ni kuprove tu kwa watu kwamba hii kitu ni kweli na iki hivyo.

Kuhusu Profesa Jay

Huyu Profesa wa sasa hivi ambaye namuona, namuona kabisa anashindana na akina Shetta wakati akina Shetta ni watu ambao wanatakiwa kujifunza kwake naona kama hajui thamani yake, yaani amefika sehemu halafu anashuka tena chini, nashindwa kuelewa. Simwelewi.

Kuhusu alichogundua kwenye Academy ya wasanii ya Kili Music Awards

Mimi nimegundua tayari kuna watu ambao wameshaambiwa matokeo kwahiyo wanaona kabisa hawana shida na nimegundua kwamba kuna watu wanaogopa kusema sababu tayari wameshaahidiwa vitu fulani kwahiyo wamekaa tu kimya hawawezi kusema chochote. So sisi tulionekana tunasema kwasababu tunaona kabisa hatuoni mbele.

Kuhusu anachofanya Australia

rama 3

Australia mimi nina bendi yangu kabisa huwa nafanya kila Ijumaa na Jumamosi. Huwa pale natumia sana lugha ya Kiswahili kwasababu wazungu wanapenda sana kitu tofauti na lugha kutoka nchi tofauti ili kuweza kujifunza nao.

Kuhusu ujio wake wa Tanzania

Nimekuja kusalimia, sasa hivi makazi yangu ni Australia. Nimeshanunua pale nyumba, nimeshanunua gari mimi na wife wangu, tuna mtoto pale, yaani kila kitu ni pale sasa hivi.

Mtoto wa Rama Dee
Mtoto wa Rama Dee

Kuhusu nyimbo mpya

Yaani hapa nipo studio, nikimaliza wimbo leo (May 3), kesho Adam anafanya video, kesho kutwa unatoka kama nisipomaliza leo basi next week ntatoa.

Msikilize zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW