Bongo5 ExclusivesBurudaniMichezo

Exclusive: Kocha wa Azam FC Kupigwa Chini Leo

Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Azam FC, Stewart Hall anatarajiwa kuvunjiwa mkataba wa kuinoa timu hiyo ya wana Lamba lamba muda wowote leo hii. Kwa mujibu wa habari za chini ya kapeti zilizoifikia B5, kikao cha bodi ya timu ya Azam FC kilikaa jana katika maeneo ya Uwanja wa nyumbani wa Azam FC, Mbagala Chamazi ambapo maamuzi yalifikiwa kumtema kocha huyo.

Sababu kubwa iliyopelekea kocha huyo kusitishwa kazi ni kutofikiwa kwa malengo pamoja na mafanikio yaliyokuwa yanatarajiwa, ikiwemo ubingwa wa Kagame pamoja na kuwa kocha huyo aliboreshewa mazingira ya ufanyaji kazi.

Kocha huyo kutoka Uingereza alijiunga na Azam miaka kadhaa iliyopita akitokea Zanibar ambapo ndipo alikuwa na mkataba wa Kwanza na,Zanzibar Footbal Association, ZFA, akiinoa timu za Taifa za kisiwa hicho kabla ya kuchukuliwa na Azam FC hadi sasa ambapo mkataba unakaribia kuvunjwa.

Jitihada za kuwapata viongozi wa Azam FC zinaendelea kufanyika ambapo tutawahabrisha yatakayojiri

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents