Lady Jay Dee

Exclusive: Lady Jaydee’s Nothing But The Truth Album Review (track by track)

Mpaka sasa nyimbo mbili za awali, Joto Hasira na Yahaya zinafahamika vyema hivyo uchambuzi wangu utajikita kwenye nyimbo zingine zilizopo kwenye albam hii. Pamoja na nyimbo, albam hii ina intro na outro ambapo Jaydee anaelezea jina la Nothing But The Truth.

382624_10151392981425025_649755324_n

4. Njiwa

Njiwa ni wimbo wa mapenzi wa taarab ambao awali uliimbwa na Patricia Hillary. Ni wimbo mzuri ambao Lady Jaydee ameutendea haki. Sauti ya Jaydee inasikika vizuri na anazimudu vyema sauti za ‘mitetemo’ za waimbaji wa Taarab. Kama wewe ni mpenzi wa Taarab huu ni wimbo wako.

5. Nimekusemahe

Jaydee ameamua kuurudia wimbo wa zamani wa mkongwe wa muziki nchini, Hamsa Kalala na kuutendea haki. Kama kawaida Jaydee huwa hafanyi kosa katika kurudia nyimbo za wasanii wakongwe.

6. Historia

Historia ni wimbo mfupi na wenye mahadhi ya Rhumba. Katika wimbo huu Jaydee anatoa funzo kwa watu kujipanga mapema ili siku itakapofika waweze kuwa na historia nzuri. “Unakubalije uwe historia kabla siku yako haijaifika,” anaimba Jaydee kwenye wimbo huu

7. Tell Him

Kwenye Tell Him Jaydee anaimba kile akiwezacho zaidi, slow. Tell Him ni wimbo mzuri wa mapenzi unaoweza kukufanya mwili usisimke wakati ukiusikiliza. Nimependa sana piano inayopigwa kwa ustadi kwenye wimbo huu. Ngoma hii imetengenezwa kwenye studio za B’Hits Music Group na ambapo executive producer ni Hermy B. Piano imepigwa na Elisha.

Piano hiyo inanikumbusha enzi za Machozi. “Tell him I love him, tell him i need him, tell him I care I will be there,” anaimba Jaydee kwenye chorus ya wimbo huu. Kama unataka kumsikia Lady Jaydee wa zamani huu ni wimbo wa kuusikiliza.

Pamoja na piano tamu inayotambaa vizuri na sauti ya Jaydee kwenye wimbo, kuna gitaa zuri linasikika likiwa ‘panned’ kwenye siku moja (utalisiKia vizuri ukiwa na headphone) ambalo limecharazwa na mtu mwingine pia. Kuna strings za kuvutia pia zinasikika zikiwa panned zilizopigwa na producer mkongwe, Bizman.

Jaydee anakuja kubadilika kwenye bridge na kupokelewa na ‘distorted guitar’ lililokuwa panned pia na linaloimba kama limecharazwa na Carlos Santana na Jaydee anasikika akitranspose (kuhama key) baada ya bridge. Huu ni wimbo mkali sana.

8. When You Cry

Kwenye ngoma hii iliyotengenezwa na Fishcrub Cookout, Jaydee anasikika akilalamika kwenye beat moja kali ya Hip Hop. Kuna piano tamu pia zinasikika kwenye ngoma hii. Ni wimbo wa mapenzi pia.

9. Tell Him Remix ft Xtatic

Remix ya Tell Him yote imetengenezwa na Hermy B ambaye alihisi kuna umuhimu wa kutengeneza version iliyochangamka zaidi (club version) ya Tell Him ili kuipa uhai wa ziada. Kwenye remix hii ameshirikishwa rapper wa kike wa Kenya, Xtatic aliye chini ya label ya Sony Music Africa. Xtatic amechana poa sana na nahisi wimbo huu kama ukitoka unaweza ukaenda mbali zaidi na kumpa mashavu makubwa Jide. Nimependa jinsi Hermy B alivyoibadilisha beat hii kuanzia dakika ya 2:53 na kuipa ladha nyingine ya kuchezeka zaidi.

10. Msichoke ft Machozi Band

Kwenye wimbo huu Jaydee amewapa shavu vijana wake wa Machozi Band walilolitumia vizuri.

Nothing But The Truth ni albam kali. Sikiliza vipande vya nyimbo hizo hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents