Burudani

Exclusive: Linah akanusha kubakwa, ‘sijapenda, ni bora mtu anizushie kitu kingine lakini si hilo (Audio)

Mrembo na mwanamuziki wa kike nchini, Linah Sanga amezikanusha ripoti zilizosambazwa leo kuwa amebakwa na rapper Kimbunga na kudai kuwa ameshangazwa mno na taarifa hizo.

edd702e8e8af11e286e122000a9e080f_7

Taarifa hizo zimeanza kusambazwa leo mchana baada ya akaunti ya Facebook inayoonekana kuwa ya rapper Kalapina yenye jina ‘KalApina Kikosi Cha Mizinga’ kuandika:

“Mtoto kimbunga amechamba ana leta usela mavi mambo ya kizamani hivi yupo chini ya ulinzi osterbay police kwa kosa la kumbaka msanii lina.”

Bongo5 imezungumza na Linah ambaye amesema amepigiwa simu na watu wengi wa karibu kumuuliza suala hilo wakiwemo, Barnaba, Ditto, Amini na mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown.

Amesema Soudy alimwambia kuwa ameziona taarifa hizo kwenye Facebook kwenye akaunti ya Kalapina.

“Sasa nikasema Kalapina ameandika hivi, kwasababu sijaingia mwenyewe kuangalia chochote. Sikutaka kujipa stress kwasababu kuna kazi nafanya nisije nikaharibu kazi kwahiyo nikaona vitu vingine kama hivi ni vya kupotezea tu lakini sio vizuri kabisa yaani. Kiukweli sijapenda, yaani bora mtu anizushie kitu kingine chochote lakini si suala kama hilo hapo, si suala zuri,” amesema Linah.

Amesema jana usiku alitoka na mpenzi wake kwenda kwenye sinema na wakarejea nyumbani salama.

“Sasa sielewi huko kubakwa nimebakwa saa ngapi na nilikuwa na boyfriend wangu labda yeye ndio kanibaka! Maana mtu wanayeniambia amenibaka Kimbunga, huyo Kimbunga hata simjui, namskia tu.Nashindwa kuelewa, kwanini mtu azushe kitu kama hicho yaani ndo nataka kujua source ni nini. Niko fine yaani, kwasababu naelewa ‘it’s not true, lakini nafikiria huyo mtu mpaka kaamua kunifanyia kitu kama hicho, nimemkosea nini au kuna kitu gani, yaani hicho ndio kinaniumiza kichwa.”

Msikilize zaidi Linah hapo chini.

Hata hivyo, tumempigia simu Kalapina kumuuliza habari hizo zimetoka wapi na yeye kuendelea kusema kuwa habari hizo zimeenea maeneo mengi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu wanaendelea kudai ni habari za kweli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents