Burudani

Exclusive: M-Rap adai haitambui ngoma mpya ‘Nishike’ iliyoachiwa leo na B’Hits (Audio)

Rapper M-Rap amesema hautambui wimbo ulioachiwa leo na B’Hits kwakuwa anaamini umeachiwa ili kumharibia mipango yake.

m,rap

Rapper huyo aliyejitoa/ondolewa kwenye label hiyo wiki iliyopita aliachia wimbo mpya uitwao ‘Usiende Mbali’ aliomshirikisha Jux na kutayarishwa na AM Records na Jumatatu hii B’Hits wameachia wimbo wake mwingine mpya uitwao ‘Nishike’. “Mimi hii nyimbo sina taarifa nayo sasa sielewi sababu mimi nilishasema nimemaliza nao na nyimbo tayari nilishafanya sehemu nyingi kwahiyo hii siitambui,” M-Rap ameiambia Bongo5.

“Sawa ni yangu lakini hapo mwanzo walikataa kunipa mimi hiyo nyimbo sababu ni nyimbo ambayo mimi nilikuwa naiulizia itoke, kwahiyo mimi nilishaamua kugive up nikasema naendelea na mambo yangu mengine ilimradi tu nifanya kitu kingine kizuri,” ameongeza.

M-Rap amesema hatofanya chochote kuhusu wimbo huo kwakuwa hautambui. Msikilize zaidi M-Rap hapo chini.

Usikilize wimbo huo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents