Habari

Exclusive: Marlow azungumzia sababu za kuwa kimya, ‘nahitaji kwenda kimataifa zaidi’

Hitmaker wa Bembeleza, Marlow amesema ukimya wake wa muda mrefu umetokana na kuwa jikoni kupika nyimbo kali zaidi zitakazomfanya avuke border.

marow

Ameiambia Bongo5 kuwa anatarajia kutoa wimbo wake mpya mwezi July.

“Hii project yangu ukisikia baadhi ya nyimbo nilizofanya, hakuna wimbo wa masihala. Ninajua kabisa kuwa mimi ni role model, watu wengi wananifuatilia, kwahiyo ni lazima nijiweke sawa, mimi sihitaji kila mwezi niwe na wimbo mpya, sababu nikifanya hivyo pia nazuia soko la watu wengine, hauwezi kuwa na baraka kama huruhusu artist wengine kutokea,” amesema Marlow.

“Mimi nahitaji kwenda mbele, kama Tanzania nimeshafanya kazi nimemaliza, I need to go forward, twende na watu wengine pia watufahamu, uking’ang’ania hapa Bongo unakuja unashindana na wenzako na wasanii wengine wanatokezea hapa hapa watu wanakuona husongi mbele. Inabidi uendelee kufanya vizuri zaidi ili kusudi wao wakuone kweli unastahili kufuatwa.”

Marlow amesema kwa sasa anavutiwa zaidi na kazi za Diamond, Ben Pol na Barnaba. Msikilize zaidi hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents