Bongo5 Exclusives

Exclusive: Shaa asaini mkataba na ‘Mkubwa na Wanae’ ya Fela, kuachia wimbo ‘Sugua Gaga’ soon

Hitmaker wa Lava lava, Sarah Kaisi aka Shaa amesaini mkataba wa usamimizi wa miezi sita na kampuni ya Said Fela, ‘Mkubwa na Wanae’ akishirikiana na Babu Tale.

1011744_10151895328378570_1262274774_n

Akiongea na Bongo5, Fela amesema wameamua kumsimamia Shaa ili kumwezesha muziki wake uwafikie pia watu wa kawaida ambao kwa muda mrefu nyimbo zake za mwanzo zimekuwa zikiwabagua.

“Mimi ndio nilitoa hilo wazo, kwamba niliona Shaa anafanya kweli muziki mkubwa lakini kuna watu wanamiss vitu vyake hususan wale wa uchochoroni zaidi,” amesema Fela. “Nikamwambia Tale kama vipi tuongee na Master Jay, mimi nataka nioneshe kitu kwamba ndani ya miezi 6 atukabidhi sisi tufanye naye kazi ili tumlete kwa waswahili zaidi, Master J uzuri akatukubalia. Japokuwa mkataba wenyewe ni mfupi, lakini tunaweza kuleta mapinduzi katika muziki wetu.”

“Tutakachomwambia afanye kile tunachokiona sisi cha kufanya kama anataka kufanya mduara afanye, kama anataka kufanya mchiriku afanye, kama tutaamua afanye ‘mkinda’ au ‘mkibiji’zote hizo itabidi Shaa afanye sababu kuna watu wanahitaji sauti ya Shaa kwenye hizo ngoma za Kiswahili.”

Fela amesema kwa kuanza Shaa ataachia wimbo uitwao Sugua Gaga uliotengenezwa na Shirko.

“Magaga ni yale yanayojitokeza kwenye kisigino, kukatikatika hivi,” amefafanua Fela.

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/114538027″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Kwa upande wake Shaa ameiambia Bongo5 kuwa siku zote anapenda kufanya vitu tofauti na ndio maana ameingia mkataba huo na Fela. “Step iliyofuatia sasa ni kwamba nifanye vizuri kazi na Babu Tale na Fela ambao wao kwa pamoja wana kampuni yao ya Mkubwa na Wanaye. Nikaona sio vibaya nikiwajaribu na wao kwa pamoja sababu ni timu ambayo ni kali sana kwenye industry yetu,”amesema Shaa.

“Kwa kuanza tumesaini mkataba wa miezi 6. Ngoma ya kwanza kutoka inaitwa Sugua Gaga, lakini kuna ngoma kadhaa ambazo tumeshafanya ambazo na zenyewe zitafuata, kuna wimbo nimefanya na AT, umeandikwa na AT, kuna wimbo nimefanya na Shetta. Ni project ambayo naamini itanikeep busy sana na mashabiki wangu hawatanimiss kihivyo. Mwisho wa siku mimi kama Shaa napenda kufanya muziki ambao ni Afro-Pop Bongo Flava. Kwahiyo kwenye hii project vilevile sikutaka kukimbia sana huko, nikaona sio mbaya nikijaribu mandhari ya Mchiriku, Taarab, ambao mimi naamini bado ni Afro-Pop lakini kwajinsi nitakavyoifanya mimi ndio itakuwa KiShaa zaidi, kiAfri-Pop zaidi. Kwahiyo huu Sugua Gaga ni design hiyo,ni mchiriku zaidi.

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/114537731″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Shaa amesema tayari ameshafanya nyimbo na watayarishaji kama Marco Chali, Manecky na Shirko.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents