Burudani ya Michezo Live

Exclusive Video: Anayedai ni mdogo wake Diamond, Saleh Abdul asema ‘Diamond ananikana’

Katika pita pita zetu tumekutana na kijana aitwaye Saleh Abdul anayedai kuwa ni mdogo wake na Diamond Platnumz. Saleh anadai yeye na Diamond wanachangia baba lakini jitihada zake za kuwa karibu na kaka yake zimekuwa zikigonga mwamba kwakuwa hitmaker huyo anadai kumkana.

“Mimi ni mtu ambaye nina kipaji cha kuimba lakini najikuta kwamba naambulia patupu yaani kukosa msaada wowote, nikimwendea kaka yangu Diamond anashindwa kunielewa, hataki kunisaidia, halafu wakati mwingine ananikana kabisa kwamba mimi sio mdogo wake,” amesema Saleh kwa uchungu.

Tunafanya jitihada kumtafuta Diamond athibitishe kama kweli Saleh ni mdogo wake.Jina halisi la Diamond ni Naseeb Abdul.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW