Burudani

Exclusive Video: Ditto azungumzia kampuni yake, ukulima na sababu za ukimya

Unaweza ukawa hujamsikia Lameck Ditto kwa muda mrefu, lakini muimbaji huyo wa THT anaendelea kufanya mambo makubwa. Kwa sasa akishirikiana na Amini, wanamiliki kampuni ya masuala ya ubunifu na matangazo ambayo inafanya kazi na makampuni makubwa nchini.

“Hata nisiposikika sauti yangu kwenye redio, vipo vitu vingine chini ambavyo naendelea navyo lakini ndani ya muziki humo humo,” Ditto ameiambia Bongo5. “Ninayo kampuni ambayo tunashare mimi na Amini, Greenlight Music, inafanya matangazo mengi sana mimi nakuwa nyuma kule, nafanya ubunifu tofauti tofauti, nafanya voice-over nyingi sana, vipindi vingi katika TV zinasikika, lakini hata matangazo mengine makubwa tu yanahithit, zote ni kazi ambazo nazifanya.”

Ditto amesema kuna watu waliogundua kipaji chake cha ubunifu tofauti na kuimba tu na akaamua kuchukua kama changamoto na kuifanyia kazi kwa takriban mwaka mmoja na ndipo alipoamua kuanzisha kampuni.

Katika hatua nyingine, Ditto amesema kwa sasa ameamua kuwekeza kwenye kilimo na sasa anamiliki shamba la ekali 16 wilayani Bagamoyo ambako analima mananasi. “Mimi napenda kilimo ndio maana nimeamua kuwekeza huko, ukiacha tu kukipenda na kuinvest, kilimo ni kitu kinacholipa sana kwasababu uwekezaji wake sio mkubwa sana, ni kitu ambacho kila mtu anaweza kufanya,”amesema.

Kuhusu ukimya wake, Ditto amesema si wa bahati mbaya kwakuwa muziki ni kitu anachokipenda kuliko kitu chochote.

“Ni kitu ambacho mimi nimepanga, lakini pia nina utaratibu wa namna ambavyo mimi nyimbo zangu ninazitoa. Pamoja na hivi unavyoniona lakini mimi ni mmoja wa wasanii wenye nyimbo chache sana. Ukiacha dunia ina mambo ambayo nilifanya na Afande Sele, nina nyimbo mbili tu nyingine, Tushukuru Kwa Yote na Wapo lakini miaka 10 sasa, unaniskia, tunakutana.”

Ditto amesema ataachia wimbo wake mpya hivi karibuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents