Habari

Exclusive: Stamina afungua ‘Kabwela Foundation’ kusaidia watu wenye hali ngumu

Mkali wa Hip Hop kutoka Morogoro, Stamina amesema ameamua kujikita zaidi kwenye kuisaidia jamii kwa kufungua taasisi yake, aliyoipa jina ‘Kabwela Foundation’ ili kuwafikia Watanzania wenye hali ngumu.

stamina01

Akizungumza na Bongo5 jana akiwa mkoani Morogoro, Stamina alisema anajitahidi kufanya kitu kitakachokuwa tofauti na wengine na ndio maana akaanzisha ‘Kabwela Foundation’ ambayo imesajiliwa kama kampuni itakayowasaidia watu wenye maisha magumu.

“Kabwela Foundation itakuwa na njia nyingi ya kuwafikia walengwa ambao watakuwa wamekata tamaa ya maisha ikiwa pamoja na kuwaelimisha,kuwakusanya katika makundi na kufungua miradi ya maendeleo ambayo itasimawiaw na foundation mpaka tutakapoona kundi linajiweza ndipo tutakapoliacha lijiendeshe lenyewe huku tukifuatilia maendeleo yake,”alisema Stamina.

Stamina alisema tatizo la semina nyingi za maendeleo watu wamekuwa wakitoa elimu jinsi gani ya kufanya ili ufanikiwe na kukuonyesha makampuni ya fedha ambayo yatawawezesha,lakini wanasahau elimu kwa vitendo ni nzuri zaidi,wakusanywe katika makundi ili miradi yao isimamiwe mpaka itakapokamilika kwa uthibitisho wa wataalam waliowapandikiza kwenye kila kikundi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents