Burudani

Extreme Kids Events: Tamasha la wazi la watoto, litafanyika Dar, Arusha na Mwanza

Tamasha kubwa la watoto liitwalo, Extreme Kids Events limezinduliwa rasmi wiki hii na litafanyika Dar es Salaam, Arusha na Mwanza.

PICHA NZURI KIDSSSSS edited_full
Pichani: Mwanzilishi wa Extreme Kids Festival,Bi. Ateka Ahmed na Mratibu wake, Peter Sehasiko

Tamasha hilo litafanyika Dar es Salaam May 31 hadi June Mosi mwaka huu, katika viwanja vya Leaders Club huku Arusha likifanyika October 4 hadi October 5, Mt. Meru Hotel Gardens na Mwanza litafanyika December 6 hadi December 7 mwaka huu, katika uwanja wa Nyamagana. Matamasha yote yataanza saa nne asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni.

Tamasha hilo lina lengo la kuwafikia watoto, wazazi, wanawake wajawazito, familia kwa ujumla na wote wanaotarajia kuwa na watoto baadae ili kuwasaidia kufahamu wapi wanaweza kupata bidhaa bora na huduma bora kwa ajili ya watoto, kama vile taarifa za shule bora, afya na huduma nyingine.

Meneja masoko wa Extreme Kids Events, Yvonne Moyo amesema katika tamasha hilo kutakuwa na burudani mbalimbali kwa ajili ya watoto, elimu kwa familia nzima kupitia semina pamoja na bidhaa mbalimbali kwa ajili ya watoto.

“Extreme Kids Festival ni tukio kwa ajili ya familia nzima. Sababu ya kusema ‘Extreme’, ni kwa kuwa tunataka wazazi, watoto wote na yote yanayohusu afya, madaktari, wote wanaohusika na elimu hata midoli kuwa pamoja katika tukio moja na kisha tunaweza kuwa na muziki na tamasha la familia. Hakutakuwa na pombe, na hii ni kwa ajili ya kutengeneza mazingira salama kwa ajili ya watoto na familia,” alisema Yvonne Moyo.

Ameongeza kuwa watoto wanaolengwa zaidi ni wale wenye umri wa miaka isiyozidi 12 na kwamba wameanza na majiji hayo matatu lakini lengo kubwa ni kusambaa katika mikoa yote Tanzania katika miaka ijayo kwa kuwa ni tamasha la kila mwaka. Bi. Yvonne amesema wanafanya utaratibu wa kuwakusanya watoto ambao wako mbali pamoja wale waishio katika mazingira magumu na kuwasafirisha hadi katika tamasha hilo ili nao waweze kushiriki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents