Burudani ya Michezo Live

Fabinho amkaribisha Mbappe Liverpool ”Atashinda Ballon d’Or kabla ya Neymar”

Kiungo wa Liverpool, Fabinho amemkaribisha nyota wa Paris Saint-Germain Football Club, Kylian Mbappe kujiunga na majogoo wa England.

Fabinho (right) and Kylian Mbappe played together at Monaco under Leonardo Jardim

Fabinho na Mbappe walishawahi kuwa pamoja katika klabu ya Monaco chini ya kocha Leonardo Jardim kabla kila mmoja kutimka katika njia yake.

Kitu ambacho kwa sasa anachotamani kiungo huyo wa Brazili ni kuona wanaungana tena na Mbappe, aliiambia Telefoot kuwa ”Ningelipenda kumkaribisha Liverpool.”

Image result for Mbappe to Liverpool

Hata hivyo kiungo huyo mkabaji alibashiriku kuwa Mbappe atakuja kumzidi Neymar ”Mbappe atakuja kuanza kutwaa tuzo ya Ballon d’Or kabla ya Neymar.”

Mpaka sasa Mbappe ameshafunga jumla ya mabao 18 katika mashindano yote akiwa anaitumikia PSG, huku akiisadia timu yake kutwaa kombe la Ligue 1.

Msimu huu Lionel Messi ndiyo aliyetwaa taji hilo la Ballon d’Or lakini Fabinho alikuwa anaamini huwenda lingekwenda kati ya mmoja wa wachezaji anao cheza nao Liverpool kati ya Sadio Mane ama Salah ambao walishinda ubigwa wa Champions League.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW