Michezo

Fabregas apinga taarifa za kutakiwa kuondoka Chelsea

Wikiendi hii zimezuka tetesi mtandaoni kuwa kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas ameambiwa na kocha wa timu hiyo kuwa atafute timu ya kwenda kwa kuwa hayupo kwenye mipango yake.

Fabregas

Taarifa hizo zilidai kuwa kocha huyo ametoa maneno hayo kutokana na kutoridhishwa na kiwango anachokionyesha mchezaji huyo kitendo ambacho kimemfanya apoteze namba kwenye kikosi cha kwanza.

Kupitia mtandao wa Twitter mchezaji huyo amekanusha taarifa hizo kuwa si za kweli na amedai kuwa huyo kocha huyo amemwambia kwa sasa anaangalia uwezo wake hivyo ataendelea kuitumikia klabu hiyo na kuhakikisha ikipata ushindi katika michezo yake.

Diddy

Fabregas alijiunga na klabu hiyo mwaka 2014 akitokea Barcelona, amefanikiwa kuisaidia timu hiyo kuchukuwa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza katika msimu wake wa kwanza kuichezea timu hiyo huku akifanikiwa kuongoza kwa kupiga pasi za mwisho zilizosababisha magoli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents