Uncategorized

Fabregas kuwaaga mashabiki wa Blues mbele ya Nottingham Forest, Maurizio Sarri adai bado anamuhitaji

Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas huwenda mchezo wake dhidi ya Nottingham Forest ikawa ndiyo wa mwisho katika kuhitimisha safari yake ya kuitumikia miamba hiyo ya soka ya Uingereza.

Inaelezwa kuwa, Fabregas mwenye umri wa miaka 31 mkataba wake utafikia tamati mwishoni mwa msimu huku kukiwa na taarifa kuwa Chelsea inakaribia kufikia makubaliano na miambaya soka ya Ligue 1 klabu ya Monaco kwaajili ya kumchukua kiungo huyo katika dirisha hili la usajili mwezi Januari.

Sky sources understand Fabregas is close to moving to Monaco

Fabregas anatarajiwa kucheza mechi yake ya mwisho akiwa na kikosi cha Blues leo siku ya Jumamosi dhidi ya NottinghamForest kwenye dimba la Stamford Bridge ikiwa ni mchezo wa FA Cup.

Nyota huyo amekuwa akihaha kuhakikisha anapata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza msimu huu, huku akiwa amepata nafasi ya kucheza mara sita pekee Premier League chini ya kocha, Maurizio Sarri.

Hata hivyo meneja huyo anatamani kumuona Fabregas akiendelea kusalia ndani ya Stamford Bridge huku akidai kuwa kwenye nafasi hiyo wapo wawili ambao ni yeye pamoja na Jorginho hivyo kuondoka kwake ni tatizo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents