Technology

Facebook waja na sarafu yake ya Mtandaoni, hili ni pigo kwa kampuni ya Bitcoin

Mtandao maarufu wa Facebook umetangaza kuja na sarafu yake mpya ya mtandaoni (Cryptocurrency) ambayo itakuwa inatumika kununua bidhaa mbalimbali kwenye mtandao huo.

Kwa mujibu wa mtandao wa WSJ kwa sasa facebook wameanza kuweka vigezo vya kuzuia matangazo ya kibenki ili kujiandaa na mradi huo.

Mradi huo uliopewa jina la ‘Project Libra’ unatarajiwa kuanza mwakani na hii itasaidia watumiaji wa mtandao huo kununua, kutumiana na kupokea hela.

Mtandao wa WSJ umeeleza kuwa Facebook wameanza mazungumzo na makampuni makubwa ya kibiashara ya Mastrercard na Visa Inc. ili kuwasaidia namna ya kuimarisha thamani ya sarafu hiyo.

Ujio huo ni pigo kwa kampuni ya maarufu ya sarafu mtandaoni ya Bitcoin ambayo kila siku thamani yake inashuka duniani.

Kwa sasa matangazo yote ya Bitcoin kwenye mtandao wa Facebook yameanza kuondolewa ili mtandao huo uanze kujiimarisha kibiashara.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents