Habari

Fagio la kuwaondoa wanachama wasaliti CCM laendelea

Chama cha Mapinduzi CCM kimesema zoezi la kuwaondoa wasaliti kwenye Chama kwa sasa linakwenda kwenye mashina na matawi kwa lengo la kurejesha chama chenye wanachama hai na waaminifu.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM, Alhaji Abdallah Bulembo alipokuwa akizungumza na wananchama wa CCM wilaya ya Ilala katika ziara yake jijini Dar es salaam.

“Kwanini tumepoteza madiwani ni usaliti tulioutengeneza ndani ya Chama chetu, kuwa CCM ni imani, kuwa muislam ni imani, na kuwa mkristo ni imani, sasa unapoona imani yako wewe ina utata kama unataka kwenda wewe nenda si ndio jamani, watakao kuwa na imani watazidi kubaki na imani yao,” alisema Bulembo.

“Kwahiyo kwa Dar es salaam tunayoshida na niliseme moja kwa moja hapa na popote ntakapo kwenda ntasema kabla ya agenda yangu kubwa ya uchaguzi Dar es salaam hatujamaliza na naomba nieleweke vizuri Dar es salaam hatujamaliza kuwahakiki waliokuwa wasaliti, tutakuja hadi kwenye matawi.”

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilifanya mkutano mkuu maalumu Machi 12, mwaka huu mkoani Dodoma ambapo waliwatimua wanachama walio kisaliti chama hicho.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents