Afya

Fahamu dalili kuu za ugonjwa wa kisukari

Ni kama mwezi mmoja umepita ambapo tulikujuza kuhusu aina kuu mbili za ugonjwa wa kisukari ambazo ni:-Insulin -dependent na Insulin-independent.

Leo kupita Bongo5 tutakujuza kuhusu baadhi ya dalili kuu za ugonjwa wa kisukari.

Baadhi ya dalili kuu za kisukari ni:
• Kiu iliyozidi
• Kukojoa mara kwa mara
• Kupatwa na ganzi kwenye miguu na mikono
• Kujisikia mchovu
• Kutoona vizuri
• Kuongezeka njaa
• Kushindwa kuhimili tendo la ndoa.
Ikiwa daktari atakuona una dalili za kuwa na kisukari, ata kutaka ufanye jaribio la kuiandaa glukozi katika usawa wake wa chini kabisa kwenye damu (fasting plasma glucose test – fpgt), kwa sababu hiyo, atakutaka ubaki bila kula kitu chochote kwa muda usiopungua masaa nane kabla ya kukupima, ambapo kwa kawaida huwa ni asubuhi ili kupata uwezekano wa damu sukari kuwa katika usawa wake wa chini kabisa.
Kisha atachukua damu toka kwenye mkono na kuipima na kulinganisha matokeo na uwiano ufuatao:
• Chini ya 5.5 mmol/l ni kawaida
• 5.5 mmol/l – 7 mmol/l ni hatua za mwanzo za kisukari
• Zaidi ya 7 mmol/l ni kisukari.
Kisukari ambacho hakikudhibitiwa kinaweza kusababisha mwili kulazimika kuanza kuchoma mafuta ili kuzarisha nishati (diabetic ketoacidosis), hii kwa kawaida hutokea kwa watu wenye kisukari cha aina ya kwanza ambapo glukozi inaweza kuingia kwenye seli bila insulini.
Kitendo cha mafuta kutumika kuzarisha nishati huzarisha taka nyingi za asidi zilijulikanazo kwa kitaalamu kama ‘Ketones’.
Taka hizi (Diabetic ketoacidosis – DKA) hujijenga kwenye mzunguko wa damu na kusababisha pumzi fupi, mauzauza na kutapika na mwishowe kukuwekea koma na hata kusababisha kifo.
DKA haijitokezi sana siku hizi ahsante kwa insulini na vifaa rahisi kutumia kufuatilia damu sukari.
Wakati damu sukari inapokuwa nyingi na damu inapokuwa imetulia, nene na hafifu (hyperosmolar syndrome), husababisha kukojoa mara nyingi ili kuilazimisha sukari iliyozidi kutoka nje.
Ikitokea hivyo, utapatwa na upungufu mkubwa wa maji na unaweza kushikwa na mikakamao ya miguu, mapigo ya moyo kwenda mbio, mauzauza, msukosuko, au hata kuelekea kwenye koma.
Hii huwatokea watu wenye kisukari aina ya pili ambao hawafuatilii kujuwa kiasi cha damu sukari yao mwilini.
Moja kati ya matatizo makubwa ya kisukari ni kitendo cha kushuka kwa kiasi kikubwa cha damu sukari mwilini (hypoglycemia), hii hutokea wakati damu sukari inazarishwa kidogo kutokana na kutumia kiasi kingi cha insulini au kukaa muda mrefu bila kula chochote na huku ukiwa umetumia insulini au ulinusa harufu ya chakula fulani.
Zifuatazo ni dalili za kushuka kwa damu sukari mwilini:
• Kichwa kuuma
• Mauzauza
• Mapigo ya moyo kwenda mbio
• Kutokwa na jasho jingi
• Kuona vitu viwili katika kimoja.

Chanzo na : Fadhil Paulo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents