Technology

FAHAMU: Huduma ya SPENN inayokuwezesha kufanya miamala yako bure bila makato (+video)

SPENN ni huduma inayokujia kupitia Benki ya I&M inayokuwezesha kufanya miamala mbalimbali bure ambapo unaweza kufungua akaunti binafsi na akaunti ya biashara.

Bw. Jens Glaso ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Blockbonds na SPENN, ameelezea furaha yake kuingiza rasmi huduma hii katika soko jingine barani Afrika baada ya kufanikisha kuizindua rasmi nchini Rwanda mwaka 2018. Huduma ya SPENN imeweza kupokelewa vyema nchini Rwanda ambapo hadi sasa inawatumiaji zaidi ya 130,000 ikiwa ni kipindi kifupi tangu ilipozinduliwa rasmi.

“Lengo letu ni kuhakikisha kwamba kila mmoja anapata fursa ya huduma za kifedha kupitia teknolojia yenye ubunifu wa hali juu. Kufanikisha upatikanaji wa huduma ya SPENN nchini Tanzania ni hatua kubwa sana katika kutimiza malengo yetu ya muda mrefu”. Alisema Bw. Glaso.

Kwa kupakua App ya SPENN bure, mtu yoyote anaweza kufungua akaunti ambayo haina gharama za uendeshaji. Kila mtumiaji anaweza kutuma na kupokea pesa, kufanya malipo katika maduka mbalimbali pamoja na kuweka na kutoa fedha katika tawi lolote la Benki ya I&M.

Vile vile huduma ya SPENN inakupa suluhisho la bure la kuweza kufanya biashara yako ya kuuza bidhaa na huduma kwa ufanisi kwa kukupa njia ya rahisi ya kupokea malipo bila kutumia fedha taslimu endapo utajisajili kuwa mtumiaji wa SPENN Plus. 

Ni rahisi sana! Mtu yoyote anayemiliki simu aina ya smartphone anaweza kujisajili na SPENN kwa urahisi ambapo ili kujisajili unapaswa kuwa na namba ya simu, jina kamili pamoja na namba ya kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na NIDA.

“Kuwa na akaunti benki ni hatua ya kwanza ya kuondokana na mfumo wa uchumi unaohitaji fedha taslimu kufanya miamala na inaweza kuwa ni hatua muhimu katika kakabiliana na umaskini” alisema Bw. Glaso. “Imani yetu ni kwamba ni haki ya kila binadamu kuwa na akaunti ya benki na SPENN ni linalochangia katika kufikisha huduma za kifedha kwa watu wengi zaidi na kuchangia katika kuondokana na mfumo wa uchumi unaohitaji fedha taslimu kufanya miamala”.

“Benki ya I&M ni benki yenye ubunifu ambayo imejikita zaidi katika huduma za kidigitali na SPENN ni huduma inayolenga kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja. Huduma ya SPENN itabadilisha namna ambavyo Watanzania wanafanya miamala yao ya kifedha na kufanya mfumo mzima wa kufanya miamala kuwa na ufanisi zaidi, wenye usalama na pasipo kuwa na gharama. Tunaamini kabisa huduma ya SPENN itachangia katika kuboresha maisha ya Watanzania”, alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya I&M Bw. Baseer Mohammed.  

Ikiwa na watu zaidi ya milioni 57 sambamba na huduma ya mtandao ya haraka na gharama nafuu, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotegemewa kuwa na watumiaji wengi wa huduma SPENN.

Kuhusu Blockbonds AS

Blockbonds ni kampuni yenye makao yake makuu nchini Norway na ni waanzilishi wa huduma ya SPENN.  Huduma ya SPENN inawezesha watumiaji wake kufanya miamala ya kibenki kwa njia ya simu ya mkononi kwa kutumia teknolojia ya “blockchain” ambayo lengo lake kuu ni kuiunganisha dunia kupitia mfumo wa fedha kwa kuwaunganisha watu waliofikiwa na huduma za kibenki na wale ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki. 

Takwimu zinaonyesha kwamba watu wapatao bilioni 2 duniani kote hawatumii mfumo rasmi wa huduma za kifedha. Asilimia 73 ya watu walio kipato cha chini hawatumii huduma za kibenki kwa sababu ya gharama zinazohusiana za uendeshaji wa akaunti pamoja na mahitaji ya kufungua akaunti. SPENN ni suluhisho la kila mmoja kuwa sehemu ya mfumo wa uchumi usiohitaji fedha taslimu kufanya miamala, ambapo itamuwezesha kila mtu kupata huduma za kifedha kwa urahisi bila gharama yoyote.

Mawasiliano:

Jens Glaso, Afisa Mtendaji Mkuu na Muasisi
Barua Pepe: [email protected] 

Simu: +47 40 40 47 50
Tovuti: www.blockbonds.io
               www.spenn.com

Kuhusu Benki ya I&M.

Benki ya I&M ilianzishwa mwaka 1974 ikiwa kama taasisi ya kifedha na ilianza iliingia nchini Tanzania mwaka 2010 baada ya kuinunua iliyokua ikijulikana kama Benki ya CF Union. Katika kipindi cha miaka 8 tangu kuingia nchini, Benki ya I&M imekua miongoni mwa benki zinazofanya vizuri sokoni na kuweza kufungua matawi mapya 6 kutoka matawi mawili yaliyofunguliwa wakati wa CF Union. Matawi ya Benki ya I&M yanapatikana mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Moshi mkoani Kilimanjaro.  

  • Tawi Kuu (Main Branch) – Indira Gandhi/Mosque St, Dar es Salaam
  • Tawi la Oysterbay – Toure Drive & Ghuba Road, Dar es Salaam 
  • Tawi la Maktaba – Maktaba Square, Dar es Salaam 
  • Tawi la Nyerere – Quality Plaza , Dar es Salaam
  • Tawi la Kariakoo – Livingstone St, Dar es Salaam
  • Tawi la Arusha – Falcon Building, Jakaranda St, Arusha
  • Tawi la Moshi  – Rindi Lane, Moshi
  • Tawi la Mwanza– Gradia Tower, Uhuru Street.

Mawasiliano:

I&M Bank (T) Ltd 
Mtaa wa Maktaba

Dar Es Salaam, Tanzania

Simu: +255 22 2127330-4
Nukushi: +255 22 2127336
Barua Pepe: [email protected]

Tovuti: https://www.facebook.com/IMBankTZ/
https://twitter.com/imbanktzltd
https://www.instagram.com/imbanktz/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents