Habari

Fahamu jiko linalotumia moto wa mawe ya kusugulia miguu lilobuniwa na kijana wa Mwanza, linaivisha Maharage kwa dakika 15  

Omap ikiwa na maana ya ‘okoa mazingira na pesa’, ni aina ya jiko lililobuniwa na Shabani Machemba kutoka jijini Mwanza, Tanzania.

jiko

Jiko hilo linalotumia mawe ambayo ni mabaki ya voclano ambayo ni maarufu kwa wengi kama mawe ya kusugulia miguu. Jiko hili lina mfumo wa upepo unaotumia umeme wa jua kujiendesha.

Ubunifu wa jiko linalotumia makaa ya mawe

Upepo wa kutosha huyawezesha mawe haya kuwaka bila ya kuzima.

Namna ambavyo jiko hili linatumika

Ili mawe haya yaweze kuwaka baada ya kuwekwa jikoni lazima yachanganywe na chenga kidogo za mkaa chenga ili kuyasaidia yashike moto.

Baada ya hapo huendelea kuwaka yenyewe yakitegemea zaidi hewa ya oksijeni inayofuliwa na feni iliyopo upande wa chini wa jiko kwenye kiboksi maalumu.jiko

Mawe yanayotumika kama mkaa katika jiko hili maalum

Kwa mujibu wa mbunifu huyu fungu moja la mawe linalouzwa kwa wastani wa dola moja hadi mbili yanaweza kutumika kwa kipindi cha miezi sita bila ya kuisha hata kama mtumiaji akifululiza kupika vyakula vinavyo chukua muda mrefu kama vile maharage.

Jiko hili ambalo linaendelea kuwashangaza wengi, linaweza kuchemsha maharage kwa kipindi cha dakika 15 tu na yakawa yameiva kabisa.jiko

Jiko la makaa ya mawe

Wakati anaanza ubunifu huu,Shabani anasema kuwa aliharibu majiko mengine matano akihangaika kukamilisha ubunifu huu ambao sasa anafanya kwa ufanisi ingawa bado anaendelea na maboresho kila siku.

Ni takribani miaka miwili tangu Shaban aanze kutengeneza majiko haya na sasa anaweza kutengeneza kwa ukubwa mbalimbali kutokana na mahitaji ya mteja.

Jiko moja linagharimu kati ya shillingi laki moja na nusu mpaka laki mbili za Tanzania sawa na dola 70 mpaka dola 100.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents