Tupo Nawe

Fahamu jinsi kifaa cha kuzuia mimba kilivyowalemaza wanawake nchini Ireland, wanawake wasimulia

Fahamu jinsi kifaa cha kuzuia mimba kilivyowalemaza wanawake nchini Ireland, wanawake wasimulia

Alana Nesbitt anahisi kama ni kisu kilichomo ndani yake, lakini kifaa hiki kiliwekwa na daktari. Alana ni mmoja wa wanawake kadhaa ambao maisha yao yamegeuka na kuwa magumu baada ya kupandikiziwa kifaa cha Coil ndani ya mirija ya inayokutanisha mbegu ya kiume na yai la uzazi kwa ajili ya utungwaji wa mimba.

Kifaa hicho kinachofahamika kwa lugha ya kitalaamu kama Essure coil implant kimetengenezwa mahsusi kwa ajili ya kuzuwia mayai ya uzazi kuingia katika mfuko wa uzazi.

Kifaa hicho kiliondolewa kwenye soko la Uingereza mnamo mwaka 2017. Watengenezaji wa kifaa hiki , Bayer Healthcare Pharmaceuticals, walisema kuwa uamuzi wa kukiondoa kwenye maduka ya dawa na hospitali ulikuwa ni ”wa kibiashara”

Kufikia mwezi Januari mwaka huu ,uuzaji na usamabazaji wa kifaa cha Essure ulipigwa marufuku nchini Marekani, baada ya masharti makali ya matumizi yake kuwekwa na taasisi ya Marekani ya Chakula na utoaji wa dawa (FDA).

Hata hihvyo , watoaji w ahuduma za afya bado wanaweza kupandikiza kifaa cha Essure Coil kwa kipindi cha hadi mwaka mmoja tangu kiliponunuliwa.

Awali zilizuwiwa kutumiwa, kwani wanawake wengi walipata maumivu makali na wengi hadi sasa bado wanaumia kutokana na Coil.

Alana NesbittHaki miliki ya pichaALANA NESBITT
Image captionAlana Nesbitt anasema hakupata maumivu mara moja baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa kupandikiziwa Essure Coil mwilini

Alana Nesbitt, mwenye umri wa miaka 39, kutoka magharibi wa Belfast, anasema unapowekewa kifaa hicho cha kupandikizwa “unahisi kama una kisu ndani yako -ni kibaya sana”.

Bi Nesbitt ambaye ni mama wa watoto wawili anasema kuwa ,maumivu yalianza miezi michache baada ya kupandikiziwa coil mnamo mwaka 2012.

Mwanzo alikwenda kwa daktari akiwa anashuku maumivu ya kidole tumbo(appendix), lakini baadae ilibidi aagizwe kumuona daktari bingwa wa magonjwa ya uzazi kwa ajili ya matibabu.

Kwa sasa anasubiri kufanyiwa upasuaji wa kuondoa kifaa hicho.

“Kusema ukweli ni vigumu kuishi nacho ,”aliiambia BBC.

” Unakua ukifikiri kuwa hatimae utafikia umri wa ukomo wa uzazi, lakini hujui utakayoyapitia kabla ya muda huo.

“Nilifahamu kuwa ninataka kupewa kinga ya ujauzito, lakini sikufahamu nitapata maumivu ya kiasi gani. Natamani kungekuwa na taarifa na utafiti unaotolewa wakati mtu anapotaka kupata huduma hii

“Badala yake nilishauliwa niamini kuwa ni upasuaji wa haraka utakaochukua dakika 10 tu ninaoweza kufanyiwa wakati wa chakula cha mchana, na kukamilika na hiyo ndiyo taarifa tu niliyopata .”

Amy Speers, mama wa watoto wanne kutoka eneo la Bangor, County Down,pia anasubiri upasuaji wa kuondolewa kwa Assure Coil mwilini mwake.

Amy Speers
Image captionAmy Speers alipandikiziwa kifaa cha Assure Coil miaka mitano iliyopita

Alipandikiziwa Essure imwaka 2014, baada ya kuamua kuwa familia yake imekamilika.

“Ni sawa na uchungu wa kujifungua, mara nne zaidi, wote kwa wakati mmoja ,” alisema mama wa miaka 33.

“Maumivu huwa yanaongezeka unapoinama chini, wakati mwingine ukitembea unachechemea kutokana na maumivu makali .”

Vifaa vidogo huingizwa katika mirija ya fallopian ambamo husababisha majeraha, kusababisha kovu ambalo baadaye huvimba na kuziba mirija ya fallopian hali ambayo hujulikana kama hysteroscopic sterilisation.

“Maumivu unayoyapata ni kama unadungwa kisu kwa ndani, kupigwa na umeme, au kama una ujauzito usio na mimba – Nisingependa mtu yeyote apitie” Bi Speers aliiambia BBC News.

“Linakuwa ni jambo la siri, na kufunikwa chini ya zulia, lakini kupandikiziwa kifaa cha kuzuwia ujauzito – sterilisation ni kitu kibaya nilichowahi kukifanya . Afya yangu ya akili ni kama ilishuka chooni .”

Tembe za kuzuwia mimbaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTembe za kuzuwia mimba

Kumekuwa na matukio machache ya ripoti za wagonjwa wa Ireland kaskazini , kulingana na msemaji wa Wizara ya Afya ya Irleand Kaskazini.

Wizara ya Afya nchini humo inasema iliwashauri maafisa wa afya na huduma za kijamii kuwa Essure hilipoteza kibali cha matumizi yake mwaka 2017 na kuomba vifaa vilivyobakia visitumiwe.

Lakini Bayer Healthcare Pharmaceuticals, kampuni inayohtengeneza vifaa hivyo, imeiambia BBC News kwamba wanawake ambao bado wanavifaa hivyo mwilini mwao wanaweza kuendelea kuvitegemea kwa kuzuwia ujauzito.

Kelly George, kutoka eneo la County Down, aliwekewa kifaa cha Essure mwaka 2014, baada ya kuzaliwa kwa mtoto wake mdogo wa kiume. Kuanzia wakati huo alianza kupata upele anaposhika vifaa vilivyotengenezwa kwa madini ya aina ya Nikel ambayo hutumika kutengeneza kifaa cha Essure

“Nilikuwa sawa mwanzo, lakini baadae nikaanza kutokwa na jasho usiku na baada ya wiki chache ngozi yangu ikaanza kubabuka ,” aliiambia BBC News NI.

“Pia nimekuwa sijisikii vizuri tu – Niko katika sayari nyingine na kabla sikuwa hivi . Ni moja ya dalili ambazo watu wengi wamekuwa wakilalamikia kuhusu kifaa hiki .”

Bi George alifanyiwa upasuaji wa kuondoa mirija ya fallopian tubes mwezi wa Novemba na akafanyiwa upasuaji wa kuondoa kifaa Ijumaa iliyopita. “Kimeathiri vibaya maisha yangu .”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW