Fahamu

Fahamu jinsi mbwa huyu alivyookoa maisha ya mtoto mchanga aliyezikwa hai na mama yake

Fahamu jinsi mbwa huyu alivyookoa maisha ya mtoto mchanga aliyezikwa hai na mama yake

Mbwa mmoja nchini kaskazini mwa Thailand amemuokoa mtoto mchanga aliyekuwa amezaliwa baada ya kuzikwa hai anayedaiwa kuzikwa na mwanamke mwenye umri mdogo. Mwili wa mtoto huyo mchanga wa kiume unasemekana ulikuwa umezikwa na mama mwenye umri wa miaka , 15, ambaye alikuwa amewaficha wazazi wake ujauzito.

Kwa mujibu wa BBC. Mbwa kwa jina Ping Pong alionekana akiwa anabweka na kuchimba ardhini kwenye shamba katika kijiji cha Ban Nong Kham.

Mmiliki wake anasema aliposogelea mahali alipokuwa ndipo alipoona mguu wa mtoto mchanga ukitokezea juu ya ardhi.

Wanakijiji walimkimbiza mtoto hospitalini ambako madaktari walimuogesha na kutangaza kuwa alikuwa mzima wa afya.

Mmiliki wa mbwa Ping Pong , Usa Nisaikha, anasema mguu wa mbwa hake hauna nguvu baada ya kugongwa na gari.

Aliliambia gazeti la Khaosod : ” Ninamtunza kwasababu ni mwaminifu sanana kila mara huwa ananisaidia ninapokwenda shambani kuwahudumia mifugo wangu. Anapendwa sana na kijiji kizima.

Inashangaza.”

Mbwa Ping Pong amekuwa mlemavu wa mguu tangu alipogongwa na gariHaki miliki ya pichaKHAOSOD

Mama yake mtoto huyo mchanga amekwishashtakiwa kwa kumtelekeza na kujaribu kumuua.

Panuwat Puttakam, afisa lkatika kituo cha Chum Phuang, alililiambia gazeti la the Bangkok Post kuwa sasa mama huyo anahudumiwa na wazazi wake pamoja na mtaalamu wa kisaikolojia.

Alisema anajutia matendo yake.Wazazi wa msichana wameamua kumlea mjukuu wao.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents