Fahamu jinsi watuhumiwa wa mauaji ya California, walivyotoroka jela kupitia shimo la inchi 22 – Video

Fahamu jinsi watuhumiwa wa mauaji ya California, walivyotoroka jela kupitia shimo la inchi 22 - Video

Polisi wametoa picha zinazoonesha washukiwa wawili wa mauaji wakivuta kizuizi cha gereza katika jimbo la California. Santos Samuel Fonseca, mwenye umri wa miaka 21, na Jonathan Salazar, mwenye umri wa miaka 20, walitambaa na kupenya katika shimo la inchi 22 ambalo walilitoboa katika choo cha jela katika mji wa Salinas, kusini mwa San Francisco.

Ofisi ya mkuu wa Kaunti ilisema kuwa vijana hao walitumia eneo ambalo walitambua kuwa “watu hawawezi kuwaona “. wakitoroka

Wawili hao walikuwa wanasubiri mashtaka mawili tofauti dhidi yao walipoamua kutoroka siku ya Jumapili.

“Tumesikitika sana kwamba kuna watu waliokuwa wanashtakiwa kwa mauaji ambao hawapo tena katika gereza letu ,” Alisema msemaji wa ofisi ya Mkuu wa kaunti ya Monterey Jonathan Thornburg

The 22in (55cm) wide hole the murder suspects cut and crawled through at the jail in Monterey CountyShimo lenye upana wa sentimita 55 au inchi 22 ambalo washukiwa wa mauaji walilikata na kulitumia kupenya kwa kutambaakatika gereza la kaunti ya Monterey

Maafisa wanawasaka washukiwa hao, wanaoaminiwa kuwa wana silaha na ni hatari.

Ofisi ya Kaunti imetangaza kutoa zawadi ya $5,000 kwa yeyote atakayetoa taarifa kuhusu ni wapi walipo washukiwa hao.

Washukiwa walitoroka vipi?

Washukiwa walichimba shimo katika choo ambapo walinzi wa gereza wasingewaona, maafisa wamesema.

Shimo hilo lilikuwa ni pana vya kutosha kwa Bwana Fonseca na Bwana Salazar, wote wakiwa na urefu wa mwili wa futi 5 na inchi 7 (1.7m) kuweza kupanda na kupenya.

A picture showing a hole in the ceiling of a jail's toilet, where two suspects climbed throughMaafisa wamesema kuwa washukiwa walibaini ” eneo ambalo haliangaliwi” katika choo cha jela

Eneo walilochimba lilikuwa na shuguli za ukarabati zilizofanya eneo hilo kujaa mabomba na nyaya.

Washukiwa walitambaa kupitia eneo hili ambalo linasemekana lilikuwa na upanda wa inchi 11- hadi walipofika kwenye mlango wa chuma, ambao waliusukuma hadi ukafunguka na kutoroka .

The maintenance area where two suspects crawled throughWashukiwa walijiburuza kwa kutambaa kupitia enepo lililokuwa likifanyiwa ukarabati baada ya kupanda kupitia shimo walililolitoboa

Unaweza pia kusoma:

Mlango wa chuma ulikuwa nyuma ya gereza, ambako hakuna uzio wa usalama uliozungushwa kwa waya, wamesema maafisa.

Walikuwa wanakabiliwa na mashtaka gani?

Washtakiwa hao wawili walikamatwa na kushtakiwa mwaka jana kuhusiana na kesi mbili tofauti za mauaji, wamesema maafisa.

The hatch through which the suspects escapedMlango wa chuma ambao waliutumia kutoroka

Bwana Fonseca anashutumiwa kumuua Lorenzo Gomez Acosta, mwenye umri wa miaka 37, na Ernesto Garcia Cruz mwenye umri wa miaka , 27 siku nne tofauti mwezi Juni 2018.

Bwana Salazar anashutumiwa kwa kumpiga risasi Jaime Martinez, aliyekuwa na umri wa miaka 20, Oktoba, 2017.

Washtakiwa wote wawili walikana mashtaka dhidi yao, kwa mujibu wa gazeti la Los Angeles Times.

Unaweza pia kusoma:

Mpango wa mfungwa kutoroka jela kijanja watibuka

Chanzo BBC

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW