Fahamu

Fahamu kisa hiki cha mwanaume aliyeuona mguu wake uliokatwa kwenye pakiti la Sigara

Fahamu kisa hiki cha mwanaume aliyeuona mguu wake uliokatwa kwenye pakiti la Sigara

Mwanamume wa miaka 60 nchini Ufaransa anasema kuwa alishangaa kuona picha ya mguu wake uliokatwa imetumiwa kwenye paketi za sigara, ikionya watu kuhusu madhara ya uvutaji sigara bila idhini yake. Picha hiyo imechapishwa kwenye pakiti hizo ikiandamana na ujumbe unaosema “uvutaji sigara unaziba mishipa ya damu”.

Lakini mtu huyo raia wa Albania, ambaye anaishi katika mji wa Metz, mashariki mwa Uganda anasema kuwa mguu wake ulikatwa baada ya kupigwa risasi mwaka 1997 nchini Albania.

Kwa mujibu wa BBC. Tume ya Ulaya ambayo inahusika na utumiaji wa picha kama hizo inasema, mtu huyo huenda amefananisha picha hiyo na mguu wake.

Mwana wa kiume wa mtu huyo aligundua picha hiyo iliyo na makovu ya jeraha la kuchomwa na moto – aliponunua paketi ya sigara mwaka jana mjini Luxembourg, vinaripoti vyombo vya habari vya Ufaransa.

Alipeleka paketi hiyo nyumbani kuonesha familia yake.

“[Ndugu ya babangu] alipofika nyumbani kutoka Luxembourg aliwekelea paketi ya sigara juu ya meza bila kusema jambo lolote ,” Binti ya mtu huyo aliliambia gazeti la Le Républicain Lorrain.

“Tulishangaa. Hatukuamini.”

Familia ilidhani moja kwa moja ni picha ya mguu wa baba yao.

“Ni baba yetu. Majeraha yake hayafichiki,” Biti huyo aliendelea kusema.

Mtu huyo ambaye jina lake limebanwa,anasema hakuwahi kutoa idhini picha hiyo itumike.

Anaamini picha hiyo ilipigwa katika moja ya hospitali nchini humo mwaka 2018 alipoenda kuulizia kama anaweza kutengenezewa mguu bandia utakaomsaidia kutembea.

Amekuwa akitembea kwa kutumia magongo kwa zaidi ya miaka 20 baada ya kupata ajali katika kisa cha ufyatulianaji risasi kilichokea mwaka 1997 nchini Albania in 1997, amabpo alipoteza mguu wake.

Usaliti

Wakili wa familia, Antoine Fittante, pia anasisitiza kuwa picha hiyo ni ya mguu wa mteja wake.

“Kila jeraha linaonekana kuwa lake kawasabu ni za kipekee. Mtu huyu pia ana alama ya kuchomeka katika mguu wake wa pili, ambayo inaonekana wazi.

Mtaalamu hatakua na wakati mgumu kutambua picha hiyo.

“Ni jambo la kusikitisha sana kwa mtu kuona picha yake katika imetumiwa katika paketi ya sigara katika mataifa ya Ulaya bila idhini yake,” Bw Fittante alisema.

“Mteja wangu anahisi kusalitiwa, na ameumia sana kimawazo kuona ulemavu wake unachapishwa katika paketi ya sigara; kusema kweli hili sio jambo zuri.”

Bw. Fittante ameandikia barua hospitali hiyo kubaini jinsi picha hiyo ilivyoishia kutumiwa.

CHANZO:https://www.bbc.com/swahili/habari-49036869

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents